Na tazama, akatoka mtu wa Mungu katika Yuda kwa neno la BWANA, akafika Betheli. Naye Yeroboamu alikuwa akisimama penye madhabahu, afukize uvumba.
Zaburi 90:1 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Wewe, Bwana, umekuwa makao yetu, Kizazi baada ya kizazi. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Ee Bwana, tangu vizazi vyote, wewe umekuwa usalama wetu. Biblia Habari Njema - BHND Ee Bwana, tangu vizazi vyote, wewe umekuwa usalama wetu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Ee Bwana, tangu vizazi vyote, wewe umekuwa usalama wetu. Neno: Bibilia Takatifu Bwana, wewe umekuwa makao yetu katika vizazi vyote. Neno: Maandiko Matakatifu bwana, wewe umekuwa makao yetu katika vizazi vyote. BIBLIA KISWAHILI Wewe, Bwana, umekuwa makao yetu, Kizazi baada ya kizazi. |
Na tazama, akatoka mtu wa Mungu katika Yuda kwa neno la BWANA, akafika Betheli. Naye Yeroboamu alikuwa akisimama penye madhabahu, afukize uvumba.
Uwe kwangu mwamba wa makazi yangu, Ngome imara ya wokovu wangu. Maana wewe, Ndiwe mwamba wangu na ngome yangu.
Fadhili za BWANA nitaziimba milele; Kwa kinywa changu nitavijulisha vizazi vyote uaminifu wako.
Naye atakuwa ni mahali patakatifu; bali ni jiwe la kujikwaza na mwamba wa kujikwaa kwa nyumba za Israeli zote mbili, na mtego na tanzi kwa wenyeji wa Yerusalemu.
basi nena, Bwana MUNGU asema hivi, Ikiwa mimi nimewahamisha, wakae katika mataifa, na ikiwa mimi nimewatawanya katika nchi kadha wa kadha, pamoja na hayo nitakuwa patakatifu kwao kwa muda mchache, katika nchi zile walizozifika.
Ee BWANA, Mungu wangu, mtakatifu wangu, wewe si wa milele? Hatutakufa. Ee BWANA, umemwandikia hukumu, nawe, Ee Jabali, umemweka imara ili aadhibishwe.
Hii ndiyo baraka ya Musa, huyo mtu wa Mungu, aliyowabarikia wana wa Israeli kabla ya kufa kwake.
Mungu wa milele ndiye makazi yako, Na mikono ya milele i chini yako. Na mbele yako amemsukumia mbali adui; Akasema, Angamiza.
Bali wewe, mtu wa Mungu, uyakimbie mambo hayo; ukafuate haki, utauwa, imani, upendo, subira, upole.
Nasi tumelifahamu pendo alilo nalo Mungu kwetu sisi, na kuliamini. Mungu ni upendo, naye akaaye katika pendo, hukaa ndani ya Mungu, na Mungu hukaa ndani yake.