Zaburi 9:4 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Kwa maana umenifanyia hukumu na haki Umeketi kitini pa enzi ukihukumu kwa haki. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Umenitetea kuhusu kisa changu cha haki; umeketi katika kiti chako cha enzi, ukatoa hukumu iliyo sawa. Biblia Habari Njema - BHND Umenitetea kuhusu kisa changu cha haki; umeketi katika kiti chako cha enzi, ukatoa hukumu iliyo sawa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Umenitetea kuhusu kisa changu cha haki; umeketi katika kiti chako cha enzi, ukatoa hukumu iliyo sawa. Neno: Bibilia Takatifu Kwa maana umetetea haki yangu na msimamo wangu; umeketi kwenye kiti chako cha enzi, ukihukumu kwa haki. Neno: Maandiko Matakatifu Kwa maana umetetea haki yangu na msimamo wangu; umeketi kwenye kiti chako cha enzi, ukihukumu kwa haki. BIBLIA KISWAHILI Kwa maana umenifanyia hukumu na haki Umeketi kitini pa enzi ukihukumu kwa haki. |
Mbele za BWANA, kwa maana anakuja, Kwa maana anakuja aihukumu nchi. Atauhukumu ulimwengu kwa haki, Na mataifa kwa uaminifu wake.
Mbele za BWANA; Kwa maana anakuja kuihukumu nchi. Atauhukumu ulimwengu kwa uaminifu, Na mataifa kwa adili.
bali kwa haki atawahukumu maskini, naye atawaonya wanyenyekevu wa dunia kwa adili; naye ataipiga dunia kwa fimbo ya kinywa chake, na kwa pumzi ya midomo yake atawaua wabaya.
Yeye alipotukanwa, hakurudisha matukano; alipoteswa, hakutisha; bali alijikabidhi kwake yeye ahukumuye kwa haki.