Zaburi 9:2 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Nitafurahi na kukushangilia; Nitaliimbia sifa jina lako, Wewe Uliye juu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Nitafurahi na kushangilia kwa sababu yako; nitaliimbia sifa jina lako, ewe Mungu Mkuu. Biblia Habari Njema - BHND Nitafurahi na kushangilia kwa sababu yako; nitaliimbia sifa jina lako, ewe Mungu Mkuu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Nitafurahi na kushangilia kwa sababu yako; nitaliimbia sifa jina lako, ewe Mungu Mkuu. Neno: Bibilia Takatifu Nitafurahi na kushangilia ndani yako. Nitaliimbia sifa jina lako, Ewe Uliye Juu Sana. Neno: Maandiko Matakatifu Nitafurahi na kushangilia ndani yako. Nitaliimbia sifa jina lako, Ewe Uliye Juu Sana. BIBLIA KISWAHILI Nitafurahi na kukushangilia; Nitaliimbia sifa jina lako, Wewe Uliye juu. |
Na sasa kichwa changu kitainuka Juu ya adui zangu wanaonizunguka. Nami nitatoa dhabihu za shangwe hemani mwake; Nitaimba, naam, nitamhimidi BWANA.
BWANA ni nguvu zangu na ngao yangu. Moyo wangu umemtumaini, Nami nimesaidiwa; Basi, moyo wangu unashangilia, Na kwa wimbo wangu nitamshukuru.
Hivyo nitakwenda madhabahuni kwa Mungu, kwa Mungu aliye furaha yangu na shangwe yangu; Nitakusifu kwa kinubi, Ee MUNGU, Mungu wangu.
Nao wote wanaokukimbilia watafurahi; Watapiga kelele za furaha daima. Kwa kuwa Wewe unawahifadhi, Walipendao jina lako watakufurahia.
Wajue ya kuwa Wewe, uitwaye jina lako YEHOVA, Ndiwe peke yako Uliye Juu, juu ya nchi yote.
Nitakusifu Wewe, Ee Bwana, Mungu wangu, Kwa moyo wangu wote, Nitalitukuza jina lako milele.
Kwa kuwa umenifurahisha, BWANA, Kwa kazi yako; nitashangilia Kwa ajili ya matendo ya mikono yako.
Maana Wewe, BWANA, ndiwe Uliye juu, Juu sana kuliko nchi yote; Umetukuka sana juu ya miungu yote.
Kwa habari zako, Ee mfalme, Mungu Aliye Juu alimpa Nebukadneza, baba yako, ufalme, na ukuu, na fahari, na utukufu;