lakini fadhili zangu hazitamwondoka, kama vile nilivyomwondolea Sauli, niliyemwondoa mbele yako.
Zaburi 89:34 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Mimi sitalivunja agano langu, Sitalibadili neno lililotoka midomoni mwangu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Sitavunja agano langu naye, wala kubatili neno nililotamka kwa mdomo wangu. Biblia Habari Njema - BHND Sitavunja agano langu naye, wala kubatili neno nililotamka kwa mdomo wangu. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Sitavunja agano langu naye, wala kubatili neno nililotamka kwa mdomo wangu. Neno: Bibilia Takatifu Mimi sitavunja agano langu wala sitabadili lile ambalo midomo yangu imelitamka. Neno: Maandiko Matakatifu Mimi sitavunja agano langu wala sitabadili lile ambalo midomo yangu imelitamka. BIBLIA KISWAHILI Mimi sitalivunja agano langu, Sitalibadili neno lililotoka midomoni mwangu. |
lakini fadhili zangu hazitamwondoka, kama vile nilivyomwondolea Sauli, niliyemwondoa mbele yako.
Nitakuwa baba yake, naye atakuwa mwanangu; wala sitamwondolea fadhili zangu, kama nilivyomwondolea yeye aliyekuwa kabla yako;
Usituchukie, kwa ajili ya jina lako; usikifedheheshe kiti cha enzi cha utukufu wako, kumbuka, usilivunje agano ulilofanya nasi.
BWANA asema hivi, Kama mkiweza kulivunja agano langu la mchana, na agano langu la usiku, hata usiwepo tena mchana na usiku kwa wakati wake,
Lakini pamoja na hayo yote, watakapokuwa katika nchi ya adui zao, mimi, sitawatupa, wala sitawachukia, niwaangamize kabisa, na kulivunja agano langu pamoja nao; kwa kuwa mimi ndimi BWANA, Mungu wao;
Kwa kuwa mimi, BWANA, sina kigeugeu; ndio maana ninyi hamkuangamizwa, enyi wana wa Yakobo.
Mungu si mtu, aseme uongo; Wala si mwanadamu, ajute; Iwapo amesema, hatalitenda? Iwapo amenena, hatalitimiza?
Kila kutoa kuliko kwema, na kila kitolewacho kilicho kamili, hutoka juu, hushuka kwa Baba wa mianga; kwake hakuna kubadilika, wala kivuli cha kugeukageuka.