Je! Sivyo ilivyo nyumba yangu mbele za BWANA? Kwa kuwa amefanya nami agano la milele; Ina taratibu katika yote, ni thabiti, Maana ni wokovu wangu wote, na shauku langu lote.
Zaburi 89:28 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Hata milele nitamwekea fadhili zangu, Na agano langu naye litadumu hata milele. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Fadhili zangu nitamwekea milele, na agano langu kwake litadumu daima. Biblia Habari Njema - BHND Fadhili zangu nitamwekea milele, na agano langu kwake litadumu daima. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Fadhili zangu nitamwekea milele, na agano langu kwake litadumu daima. Neno: Bibilia Takatifu Nitadumisha upendo wangu kwake milele, na agano langu naye litakuwa imara. Neno: Maandiko Matakatifu Nitadumisha upendo wangu kwake milele, na agano langu naye litakuwa imara. BIBLIA KISWAHILI Hata milele nitamwekea fadhili zangu, Na agano langu naye litadumu hata milele. |
Je! Sivyo ilivyo nyumba yangu mbele za BWANA? Kwa kuwa amefanya nami agano la milele; Ina taratibu katika yote, ni thabiti, Maana ni wokovu wangu wote, na shauku langu lote.
Amewapelekea watu wake ukombozi, Ameamuru agano lake liwe la milele, Jina lake ni takatifu na la kuogopwa.
Maana milima itaondoka, na vilima vitaondolewa; bali wema wangu hautaondoka kwako, wala agano langu la amani halitaondolewa; asema BWANA akurehemuye.
Tegeni masikio yenu, na kunijia; Sikieni, na nafsi zenu zitaishi; Nami nitafanya nanyi agano la milele, Naam, rehema za Daudi zilizo imara.