Zaburi 89:10 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Ndiwe uliyemponda Rahabu akawa kama aliyeuawa, Kwa mkono hodari umewatawanya wakuchukiao. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Uliliponda joka Rahabu na kuliua; uliwatawanya adui zako kwa nguvu yako. Biblia Habari Njema - BHND Uliliponda joka Rahabu na kuliua; uliwatawanya adui zako kwa nguvu yako. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Uliliponda joka Rahabu na kuliua; uliwatawanya adui zako kwa nguvu yako. Neno: Bibilia Takatifu Wewe ulimponda Rahabu kama mmoja wa waliochinjwa; kwa mkono wako wenye nguvu, uliwatawanya adui zako. Neno: Maandiko Matakatifu Wewe ulimponda Rahabu kama mmojawapo wa waliochinjwa; kwa mkono wako wenye nguvu, uliwatawanya adui zako. BIBLIA KISWAHILI Ndiwe uliyemponda Rahabu akawa kama aliyeuawa, Kwa mkono hodari umewatawanya wakuchukiao. |
Usiwaue, watu wangu wasije wakasahau; Uwatawanye kwa uweza wako, Na kuwaangamiza, Ee Bwana, ngao yetu.
Kwa hiyo wakaao mbali kabisa huogopa ishara zako; Milango ya asubuhi na jioni waifurahisha.
Mkemee mnyama wa mafunjoni; Kundi la mafahali, na ndama za watu; Hata wanyenyekee na kuleta vipande vya fedha, Uwatawanye watu wapendao vita.
Nitataja Rahabu na Babeli Miongoni mwao wanaonijua. Tazama Filistia, na Tiro, na Kushi; Wanasema, Huyu alizaliwa humo.
Tazama, BWANA ameifanya dunia kuwa tupu, aifanya ukiwa, aipindua, na kuwatawanya wakaao ndani yake.
Au Mungu amekwenda wakati gani akajitwalia taifa kutoka kati ya taifa lingine, kwa majaribu, ishara, maajabu, vita, mkono hodari, mkono ulionyoshwa, na vitisho vikuu, kama vile BWANA, Mungu wenu, alivyowatendea ninyi katika Misri, mbele ya macho yenu?