Ikawa Mungu alipoiharibu miji ya Bondeni, Mungu akamkumbuka Abrahamu, akamtoa Lutu katika maangamizi alipoiangamiza miji hiyo aliyokaa Lutu.
Zaburi 88:5 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Miongoni mwao waliokufa nimetupwa, Kama waliouawa walalao makaburini. Hao ambao Wewe huwakumbuki tena, Wametengwa mbali na mkono wako. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Nimesahauliwa kati ya wafu, kama waliouawa, walioko kaburini; kama wale ambao huwakumbuki tena, ambao wametengwa na ulinzi wako. Biblia Habari Njema - BHND Nimesahauliwa kati ya wafu, kama waliouawa, walioko kaburini; kama wale ambao huwakumbuki tena, ambao wametengwa na ulinzi wako. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Nimesahauliwa kati ya wafu, kama waliouawa, walioko kaburini; kama wale ambao huwakumbuki tena, ambao wametengwa na ulinzi wako. Neno: Bibilia Takatifu Nimetengwa pamoja na wafu, kama waliochinjwa walalao kaburini, ambao huwakumbuki tena, ambao wamekatiliwa mbali na uangalizi wako. Neno: Maandiko Matakatifu Nimetengwa pamoja na wafu, kama waliochinjwa walalao kaburini, ambao huwakumbuki tena, ambao wamekatiliwa mbali na uangalizi wako. BIBLIA KISWAHILI Miongoni mwao waliokufa nimetupwa, Kama waliouawa walalao makaburini. Hao ambao Wewe huwakumbuki tena, Wametengwa mbali na mkono wako. |
Ikawa Mungu alipoiharibu miji ya Bondeni, Mungu akamkumbuka Abrahamu, akamtoa Lutu katika maangamizi alipoiangamiza miji hiyo aliyokaa Lutu.
Na Mungu akamkumbuka Nuhu, na kila kilicho hai, na wanyama wote waliokuwamo pamoja naye katika safina; Mungu akavumisha upepo juu ya nchi, maji yakapungua;
Kwamba Mungu angekuwa radhi kuniponda; Kwamba angeulegeza mkono wake na kunikatilia mbali!
Ee BWANA, nitakuita Ewe, mwamba wangu, Usiwe kwangu kama kiziwi. Nisije nikafanana nao washukao shimoni, Ikiwa umeninyamalia.
Nami nilisema kwa pupa yangu, Nimekatiliwa mbali na macho yako; Lakini ulisikia sauti ya kilio changu Wakati nilipokulilia.
Kwa kuonewa na kuhukumiwa aliondolewa; Na maisha yake ni nani angeyajali? Maana amekatiliwa mbali na nchi ya walio hai; Alipigwa kwa sababu ya makosa ya watu wangu.
Kisha akaniambia, Mwanadamu, mifupa hii ni nyumba yote ya Israeli; tazama, wao husema, Mifupa yetu imekauka, matumaini yetu yametupotea; tumekatiliwa mbali kabisa.