Zaburi 88:11 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Fadhili zako zitasimuliwa kaburini? Au uaminifu wako katika uharibifu? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Je, fadhili zako zinatajwa kaburini, au uaminifu wako kwenye makao ya maangamizi? Biblia Habari Njema - BHND Je, fadhili zako zinatajwa kaburini, au uaminifu wako kwenye makao ya maangamizi? Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Je, fadhili zako zinatajwa kaburini, au uaminifu wako kwenye makao ya maangamizi? Neno: Bibilia Takatifu Je, upendo wako hutangazwa kaburini, uaminifu wako katika Uharibifu? Neno: Maandiko Matakatifu Je, upendo wako hutangazwa kaburini, uaminifu wako katika Uharibifu? BIBLIA KISWAHILI Fadhili zako zitasimuliwa kaburini? Au uaminifu wako katika uharibifu? |
Nawe, Ee Mungu, utawateremsha, Wafikie shimo la uharibifu; Watu wa damu na hila hawataishi nusu ya siku zao, Bali mimi nitakutumaini Wewe.
Nimechoka kwa kuugua kwangu; Kila usiku nakibubujikia kitanda changu; Nililowesha godoro langu kwa machozi yangu.
Wafu wako wataishi, maiti zangu zitafufuka; amkeni, kaimbeni, ninyi mnaokaa mavumbini, kwa maana umande wako ni kama umande wa mimea, nayo ardhi itawatoa waliokufa.
Akaniambia, Mwanadamu, je! Mifupa hii yaweza kuishi? Nami nikajibu, Ee Bwana MUNGU, wajua wewe.
Ingieni kwa kupitia mlango ulio mwembamba; maana mlango ni mpana, na njia ni pana iendayo upotevuni, nao ni wengi waingiao kwa mlango huo.
Ni nini basi, ikiwa Mungu kwa kutaka kuonesha ghadhabu yake, na kuudhihirisha uweza wake, kwa uvumilivu mwingi, alichukuliana na vile vyombo vya ghadhabu vilivyokuwa karibu kuharibiwa;
Lakini kulitokea manabii wa uongo katika wale watu, kama vile kwenu kutakavyokuwako waalimu wa uongo, watakaoingiza kwa werevu uzushi wa kupoteza, wakimkana hata Bwana aliyewanunua, wakijiletea uharibifu usiokawia.