Daudi akacheza mbele za BWANA kwa nguvu zake zote; na Daudi alikuwa amevaa naivera ya kitani.
Zaburi 87:7 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Waimbao na wachezao ngoma na waseme, Visima vyangu vyote vimo mwako. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wote wanacheza ngoma na kuimba: “Siyoni, chanzo chetu ni kwako.” Biblia Habari Njema - BHND Wote wanacheza ngoma na kuimba: “Siyoni, chanzo chetu ni kwako.” Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wote wanacheza ngoma na kuimba: “Siyoni, chanzo chetu ni kwako.” Neno: Bibilia Takatifu Watakapokuwa wanapiga vinanda wataimba, “Chemchemi zangu zote ziko kwako.” Neno: Maandiko Matakatifu Watakapokuwa wanapiga vinanda wataimba, “Chemchemi zangu zote ziko kwako.” BIBLIA KISWAHILI Waimbao na wachezao ngoma na waseme, Visima vyangu vyote vimo mwako. |
Daudi akacheza mbele za BWANA kwa nguvu zake zote; na Daudi alikuwa amevaa naivera ya kitani.
na elfu nne walikuwa mabawabu; na elfu nne walimsifu BWANA kwa vinanda, nilivyovifanya, alisema Daudi, vya kumsifia.
Kuna mto, vijito vyake vyaufurahisha mji wa Mungu, Patakatifu pa maskani zake Aliye Juu.
Baadaye akanileta tena mpaka lango la nyumba; na tazama, maji yalitoka chini ya kizingiti cha nyumba, kwa njia ya mashariki, maana upande wa mbele wa nyumba ulielekea upande wa mashariki; nayo maji yakashuka toka chini ya upande wa kulia wa nyumba, upande wa kusini wa madhabahu.
Yesu akajibu, akamwambia, Kama ungaliijua karama ya Mungu, naye ni nani akuambiaye, Nipe maji ninywe, ungalimwomba yeye, naye angalikupa maji yaliyo hai.
lakini yeyote atakayekunywa maji yale nitakayompa mimi hataona kiu milele; bali yale maji nitakayompa yatakuwa ndani yake chemchemi ya maji, yakibubujikia uzima wa milele.
Kila kutoa kuliko kwema, na kila kitolewacho kilicho kamili, hutoka juu, hushuka kwa Baba wa mianga; kwake hakuna kubadilika, wala kivuli cha kugeukageuka.
Akaniambia, Imekwisha kuwa. Mimi ni Alfa na Omega, Mwanzo na Mwisho. Mimi nitampa yeye aliye na kiu, maji kutoka chemchemi ya maji ya uzima, bure.
Kisha akanionesha mto wa maji ya uzima, wenye kung'aa kama bilauri, ukitoka katika kiti cha enzi cha Mungu, na cha Mwana-kondoo,
Roho na Bibi arusi wasema, Njoo! Naye asikiaye na aseme, Njoo! Naye mwenye kiu na aje; na yeye atakaye, na ayatwae maji ya uzima bure.