lakini nimeuchagua Yerusalemu, jina langu liwe humo; na Daudi nimemchagua awe juu ya watu wangu Israeli.
Zaburi 87:2 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC BWANA ayapenda malango ya Sayuni Kuliko maskani zote za Yakobo. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mwenyezi-Mungu anaupenda mji wa Siyoni, kuliko makao mengine ya Yakobo. Biblia Habari Njema - BHND Mwenyezi-Mungu anaupenda mji wa Siyoni, kuliko makao mengine ya Yakobo. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mwenyezi-Mungu anaupenda mji wa Siyoni, kuliko makao mengine ya Yakobo. Neno: Bibilia Takatifu Mwenyezi Mungu anayapenda malango ya Sayuni kuliko makao yote ya Yakobo. Neno: Maandiko Matakatifu bwana anayapenda malango ya Sayuni kuliko makao yote ya Yakobo. BIBLIA KISWAHILI BWANA ayapenda malango ya Sayuni Kuliko maskani zote za Yakobo. |
lakini nimeuchagua Yerusalemu, jina langu liwe humo; na Daudi nimemchagua awe juu ya watu wangu Israeli.
Wajumbe wa taifa hilo waletewe jibu gani? Ya kuwa BWANA ameiweka misingi ya Sayuni, na ndani yake wale walioonewa katika watu wake watapata kimbilio kwake.
Na itakuwa katika siku za mwisho, mlima wa nyumba ya BWANA utawekwa imara juu ya milima, nao utainuliwa juu ya vilima; na mataifa yote watauendea makundi makundi.
Na itakuwa ya kwamba mtu awaye yote atakayeliita jina la BWANA ataponywa; kwa kuwa katika mlima Sayuni na katika Yerusalemu watakuwako watu watakaookoka, kama BWANA alivyosema; na katika mabaki, hao awaitao BWANA.
Lakini mahali atakapochagua BWANA, Mungu wenu, katika makabila yenu yote, apaweke jina lake, maana, ni makao yake, elekezeni nyuso zenu hapo, nawe uende huko;