Zaburi 86:7 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Siku ya mateso yangu nitakuita, Kwa maana utaniitikia. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Siku za taabu nakuita, maana wewe waniitikia. Biblia Habari Njema - BHND Siku za taabu nakuita, maana wewe waniitikia. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Siku za taabu nakuita, maana wewe waniitikia. Neno: Bibilia Takatifu Katika siku ya shida yangu nitakuita, kwa maana wewe utanijibu. Neno: Maandiko Matakatifu Katika siku ya shida yangu nitakuita, kwa maana wewe utanijibu. BIBLIA KISWAHILI Siku ya mateso yangu nitakuita, Kwa maana utaniitikia. |
Katika shida yangu nilimwita BWANA, Na kumlalamikia Mungu wangu. Akaisikia sauti yangu hekaluni mwake, Kilio changu kikaingia masikioni mwake.
BWANA, katika taabu zao walikwenda kwako; waliomba maombi mengi wakati adhabu yako ilipokuwa juu yao.
Akasema, Nilimlilia BWANA kwa sababu ya shida yangu, Naye akaniitikia; Katika tumbo la kuzimu niliomba, Nawe ukasikia sauti yangu.
Naye kwa vile alivyokuwa katika dhiki, akazidi sana kuomba; jasho yake ikawa kama matone ya damu yakidondoka nchini.]
Yeye, siku hizo za mwili wake, alimtolea yule, awezaye kumwokoa na kumtoa katika mauti, maombi na dua pamoja na kulia sana na machozi, akasikilizwa kwa jinsi alivyokuwa mcha Mungu;