Uniwezeshe kusikia fadhili zako asubuhi, Kwa maana nimekutumaini Wewe. Unifundishe njia nitakayoiendea, Kwa maana ninakuinulia nafsi yangu.
Zaburi 86:4 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Uifurahishe nafsi ya mtumishi wako, Maana nafsi yangu nakuinulia Wewe, Bwana. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Uifurahishe roho yangu mimi mtumishi wako, maana sala zangu nazielekeza kwako ee Bwana. Biblia Habari Njema - BHND Uifurahishe roho yangu mimi mtumishi wako, maana sala zangu nazielekeza kwako ee Bwana. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Uifurahishe roho yangu mimi mtumishi wako, maana sala zangu nazielekeza kwako ee Bwana. Neno: Bibilia Takatifu Mpe mtumishi wako furaha, kwa kuwa kwako wewe, Ee Bwana, ninainua nafsi yangu. Neno: Maandiko Matakatifu Mpe mtumishi wako furaha, kwa kuwa kwako wewe, Ee bwana, ninainua nafsi yangu. BIBLIA KISWAHILI Uifurahishe nafsi ya mtumishi wako, Maana nafsi yangu nakuinulia Wewe, Bwana. |
Uniwezeshe kusikia fadhili zako asubuhi, Kwa maana nimekutumaini Wewe. Unifundishe njia nitakayoiendea, Kwa maana ninakuinulia nafsi yangu.
Enyi watu, mtumainini sikuzote, Ifunueni mioyo yenu mbele zake; Mungu ndiye kimbilio letu.
kuwaagizia hao waliao katika Sayuni, wapewe taji la maua badala ya majivu, mafuta ya furaha badala ya maombolezo, vazi la sifa badala ya roho nzito; wapate kuitwa miti ya haki, iliyopandwa na BWANA, ili atukuzwe.
Lakini furahini, mkashangilie daima, kwa ajili ya hivi niviumbavyo; maana, tazama, naumba Yerusalemu uwe shangwe, na watu wake wawe furaha.