Zaburi 85:5 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Je! Utatufanyia hasira hata milele? Utadumisha ghadhabu kizazi hadi kizazi? Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Je, utatukasirikia hata milele? Je, utadumisha ghadhabu yako kwa vizazi vyote? Biblia Habari Njema - BHND Je, utatukasirikia hata milele? Je, utadumisha ghadhabu yako kwa vizazi vyote? Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Je, utatukasirikia hata milele? Je, utadumisha ghadhabu yako kwa vizazi vyote? Neno: Bibilia Takatifu Je, utatukasirikia milele? Utaendeleza hasira yako kwa vizazi vyote? Neno: Maandiko Matakatifu Je, utatukasirikia milele? Utaendeleza hasira yako kwa vizazi vyote? BIBLIA KISWAHILI Je! Utatufanyia hasira hata milele? Utadumisha ghadhabu kizazi hadi kizazi? |
Ee Mungu, mbona umetutupa milele? Kwa nini hasira yako inatoka moshi Juu ya kondoo wa malisho yako?
Ni nani aliye Mungu kama wewe, mwenye kusamehe uovu, na kuliachilia kosa la watu wa urithi wake waliosalia? Hadumishi hasira yake milele, kwa maana yeye hufurahia rehema.
Lakini mimi, nitamtazamia BWANA; nitamngojea Mungu wa wokovu wangu; Mungu wangu atanisikia.
Wataanguka kwa ukali wa upanga, nao watatekwa nyara na kuchukuliwa katika mataifa yote; na Yerusalemu utakanyagwa na Mataifa, hadi majira ya Mataifa yatakapotimia.
ndipo ikawashwa hasira ya BWANA juu ya nchi hii, kwa kuleta juu yake laana yote iliyoandikwa katika kitabu hiki;