Biblia ya mtandaoni

Matangazo


Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya




Zaburi 85:2 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

Umeusamehe uovu wa watu wako, Umezisitiri hatia zao zote.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Umewasamehe watu wako kosa lao; umezifuta dhambi zao zote.

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Umewasamehe watu wako kosa lao; umezifuta dhambi zao zote.

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Umewasamehe watu wako kosa lao; umezifuta dhambi zao zote.

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Ulisamehe uovu wa watu wako, na kufunika dhambi zao zote.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Ulisamehe uovu wa watu wako, na kufunika dhambi zao zote.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Umeusamehe uovu wa watu wako, Umezisitiri hatia zao zote.

Tazama sura
Tafsiri zingine



Zaburi 85:2
10 Marejeleo ya Msalaba  

Koreshi, mfalme wa Uajemi asema hivi; BWANA, Mungu wa mbinguni, amenipa falme zote za dunia; naye ameniagiza nimjengee nyumba katika Yerusalemu, ulioko Yuda.


BWANA alipowarejesha mateka wa Sayuni, Tulikuwa kama waotao ndoto.


Heri aliyesamehewa dhambi, Na kuondolewa makosa yake.


Lakini Yeye, kwa kuwa anayo rehema, Husamehe uovu wala haangamizi. Mara nyingi huipishia mbali ghadhabu yake, Wala haiwashi hasira yake yote.


Katika siku hizo na wakati huo, asema BWANA, uovu wa Israeli utatafutwa, wala hakuna uovu; na dhambi za Yuda zitatafutwa, wala hazitaonekana; maana nitawasamehe wale niwaachao kuwa mabaki.


Ni nani aliye Mungu kama wewe, mwenye kusamehe uovu, na kuliachilia kosa la watu wa urithi wake waliosalia? Hadumishi hasira yake milele, kwa maana yeye hufurahia rehema.


Nakusihi, usamehe uovu wa watu hawa, kama ukuu wa rehema yako ulivyo, kama ulivyowasamehe watu hawa, tangu huko Misri hata hivi sasa.


na kwa yeye kila amwaminiye huhesabiwa haki katika mambo yale yote asiyoweza kuhesabiwa haki kwa Torati ya Musa.


Na ninyi mlipokuwa mmekufa kwa sababu ya makosa yenu na kutotahiriwa kwa mwili wenu, aliwafanya hai pamoja naye, akiisha kutusamehe makosa yote;