Zaburi 85:11 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Kweli itachipuka katika nchi, Haki itachungulia kutoka mbinguni. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Uaminifu utachipuka katika nchi; uadilifu utashuka toka mbinguni. Biblia Habari Njema - BHND Uaminifu utachipuka katika nchi; uadilifu utashuka toka mbinguni. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Uaminifu utachipuka katika nchi; uadilifu utashuka toka mbinguni. Neno: Bibilia Takatifu Uaminifu huchipua kutoka nchi, haki hutazama chini kutoka mbinguni. Neno: Maandiko Matakatifu Uaminifu huchipua kutoka nchi, haki hutazama chini kutoka mbinguni. BIBLIA KISWAHILI Kweli itachipuka katika nchi, Haki itachungulia kutoka mbinguni. |
Siku hiyo chipukizi la BWANA litakuwa zuri, lenye utukufu, na matunda ya nchi yatakuwa mema sana, na kupendeza, kwa ajili ya Waisraeli wale waliookoka.
Dondokeni, enyi mbingu, toka juu, Mawingu na yamwage haki; Nchi na ifunuke, ili kutoa wokovu, Nayo itoe haki ikamee pamoja; Mimi, BWANA, nimeiumba.
Maana alikuwa mbele zake kama mche mwororo, Na kama mzizi katika nchi kavu; Yeye hana umbo wala uzuri; Na tumwonapo hana uzuri hata tumtamani.
Alipokuwa bado akisema, tazama, wingu jeupe likawatia uvuli; na tazama, sauti ikatoka katika lile wingu, ikasema, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye; msikieni yeye.
na tazama, sauti kutoka mbinguni ikasema, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu, ninayependezwa naye.
Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.
Yeye asiyejua dhambi alimfanya kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika Yeye.