Vyombo vyote vya dhahabu na vya fedha vilikuwa jumla yake elfu tano na mia nne. Hivyo vyote Sheshbaza akakwea navyo, hapo walipokwea wale wa uhamisho kutoka Babeli mpaka Yerusalemu.
Zaburi 85:1 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC BWANA, umeiridhia nchi yako, Umewarejesha mateka wa Yakobo. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Ee Mwenyezi-Mungu, umeifadhili nchi yako; umemjalia Yakobo bahati nzuri tena. Biblia Habari Njema - BHND Ee Mwenyezi-Mungu, umeifadhili nchi yako; umemjalia Yakobo bahati nzuri tena. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Ee Mwenyezi-Mungu, umeifadhili nchi yako; umemjalia Yakobo bahati nzuri tena. Neno: Bibilia Takatifu Ee Mwenyezi Mungu, ulionesha wema kwa nchi yako. Ulimrejeshea Yakobo baraka zake. Neno: Maandiko Matakatifu Ee bwana, ulionyesha wema kwa nchi yako. Ulimrejeshea Yakobo baraka zake. BIBLIA KISWAHILI BWANA, umeiridhia nchi yako, Umewarejesha mateka wa Yakobo. |
Vyombo vyote vya dhahabu na vya fedha vilikuwa jumla yake elfu tano na mia nne. Hivyo vyote Sheshbaza akakwea navyo, hapo walipokwea wale wa uhamisho kutoka Babeli mpaka Yerusalemu.
Laiti wokovu wa Israeli ungetoka katika Sayuni! BWANA awarudishapo wafungwa wa watu wake; Yakobo atashangilia, Israeli atafurahi.
Kama ayala aioneavyo shauku mito ya maji. Vivyo hivyo nafsi yangu inakuonea shauku, Ee Mungu.
BWANA asema hivi, Tazama, nitarudisha tena hema za Yakobo zilizohamishwa, na kuyahurumia makao yake; nao mji huo utajengwa juu ya magofu yake wenyewe, nalo jumba litakaliwa, kama ilivyokuwa desturi yake.
BWANA wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Watatumia tena neno hili katika nchi ya Yuda, na katika miji yake, nitakapowarudisha mateka yao; BWANA na akubariki, Ee makao ya haki, Ee mlima wa utakatifu.
Kwa sababu hiyo, Bwana MUNGU asema hivi, Sasa nitawarejesha watu wa Yakobo waliohamishwa, nitawahurumia nyumba yote ya Israeli; nami nitalionea wivu jina langu takatifu.
Kwa maana, angalieni, siku zile, na wakati ule, nitakapowarudisha mateka wa Yuda na Yerusalemu,
ndipo nitakapokumbuka agano langu pamoja na Yakobo, tena agano langu na Isaka, tena agano langu na Abrahamu nitalikumbuka; nami nitaikumbuka nchi hiyo.
Kwa sababu hiyo BWANA asema hivi, Ninaurudia Yerusalemu kwa rehema nyingi; nyumba yangu itajengwa ndani yake, asema BWANA wa majeshi, na kamba itanyoshwa juu ya Yerusalemu.