Biblia ya mtandaoni

Matangazo

Biblia nzima Agano la Kale Agano Jipya

Zaburi 84:3 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC

Hata Shomoro ameona nyumba, Na mbayuwayu amejipatia kiota, Alipoweka makinda yake, Kwenye madhabahu zako, Ee BWANA wa majeshi, Mfalme wangu na Mungu wangu.

Tazama sura

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

Hata shomoro wamepata makao yao, mbayuwayu wamejenga viota vyao, humo wameweka makinda yao, katika madhabahu zako, ee Mwenyezi-Mungu wa majeshi, Mfalme wangu na Mungu wangu!

Tazama sura

Biblia Habari Njema - BHND

Hata shomoro wamepata makao yao, mbayuwayu wamejenga viota vyao, humo wameweka makinda yao, katika madhabahu zako, ee Mwenyezi-Mungu wa majeshi, Mfalme wangu na Mungu wangu!

Tazama sura

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

Hata shomoro wamepata makao yao, mbayuwayu wamejenga viota vyao, humo wameweka makinda yao, katika madhabahu zako, ee Mwenyezi-Mungu wa majeshi, Mfalme wangu na Mungu wangu!

Tazama sura

Neno: Bibilia Takatifu

Hata shomoro amejipatia makao, mbayuwayu amejipatia kiota mahali awezapo kuweka makinda yake: mahali karibu na madhabahu yako, Ee Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, Mfalme wangu na Mungu wangu.

Tazama sura

Neno: Maandiko Matakatifu

Hata shomoro amejipatia makao, mbayuwayu amejipatia kiota mahali awezapo kuweka makinda yake: mahali karibu na madhabahu yako, Ee bwana Mwenye Nguvu Zote, Mfalme wangu na Mungu wangu.

Tazama sura

BIBLIA KISWAHILI

Hata Shomoro ameona nyumba, Na mbayuwayu amejipatia kiota, Alipoweka makinda yake, Kwenye madhabahu zako, Ee BWANA wa majeshi, Mfalme wangu na Mungu wangu.

Tazama sura
Tafsiri zingine

Zaburi 84:3
10 Marejeleo ya Msalaba  

Naye mfalme akamwambia Sadoki, Rudisha sanduku la Mungu mjini; nikipata kibali machoni pa BWANA atanirudisha, na kunionesha tena sanduku hili, na maskani yake;

Ee nafsi yangu, urudi pumzikoni mwako, Kwa kuwa BWANA amekutendea ukarimu.

Machozi yangu yamekuwa chakula changu mchana na usiku, Pindi wanaponiambia mchana kutwa, Yuko wapi Mungu wako?

Hivyo nitakwenda madhabahuni kwa Mungu, kwa Mungu aliye furaha yangu na shangwe yangu; Nitakusifu kwa kinubi, Ee MUNGU, Mungu wangu.

Uisikie sauti ya kilio changu, Ee Mfalme wangu na Mungu wangu, Kwa maana Wewe ndiwe nikuombaye.

Wewe, Bwana, umekuwa makao yetu, Kizazi baada ya kizazi.

Aketiye mahali pa siri pake Aliye Juu Atakaa katika uvuli wake Mwenyezi.

Uwaambie nyumba ya Israeli, Bwana MUNGU asema hivi; Angalieni, nitapatia unajisi patakatifu pangu, fahari ya uwezo wenu, mahali pa kutamaniwa na macho yenu, ambapo roho zenu zinapahurumia na wana wenu na binti zenu, mliowaacha nyuma, wataanguka kwa upanga.

Ee Yerusalemu, Yerusalemu, uwauaye manabii, na kuwapiga kwa mawe wale waliotumwa kwako! Ni mara ngapi nimetaka kuwakusanya pamoja watoto wako, kama vile kuku awakusanyavyo pamoja vifaranga wake chini ya mabawa yake, lakini hamkutaka!

Yesu akamwambia, Mbweha wana pango, na ndege wa angani wana viota; lakini Mwana wa Adamu hana pa kulaza kichwa chake.