Na katika siku za Sauli wakapigana vita na Wahajiri, ambao waliangushwa kwa mikono yao; nao wakakaa katika hema zao katika nchi yote upande wa mashariki wa Gileadi.
Zaburi 83:6 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Hema za Edomu, na Waishmaeli, Na Moabu, na Wahagari, Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Watu wa Edomu na Waishmaeli, Wamoabu na watu wa Hagari; Biblia Habari Njema - BHND Watu wa Edomu na Waishmaeli, Wamoabu na watu wa Hagari; Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza watu wa Edomu na Waishmaeli, Wamoabu na watu wa Hagari; Neno: Bibilia Takatifu mahema ya Edomu na Waishmaeli, ya Wamoabu na Wahagari, Neno: Maandiko Matakatifu mahema ya Edomu na Waishmaeli, ya Wamoabu na Wahagari, BIBLIA KISWAHILI Hema za Edomu, na Waishmaeli, Na Moabu, na Wahagari, |
Na katika siku za Sauli wakapigana vita na Wahajiri, ambao waliangushwa kwa mikono yao; nao wakakaa katika hema zao katika nchi yote upande wa mashariki wa Gileadi.
Baada ya hayo, wana wa Moabu, na wana wa Amoni, pamoja nao baadhi ya Wameuni, wakaja juu ya Yehoshafati vitani.
Ee BWANA, uwakumbuke wana wa Edomu, Siku ile Yerusalemu ilipotekwa. Kwa namna walivyosema, Bomoeni! Bomoeni hata misingini!
Wafalme wa dunia wanajipanga, Na wakuu wanafanya shauri pamoja, Juu ya BWANA, Na juu ya masihi wake,
Huyo Egloni akakutanisha kwake wana wa Amoni na Amaleki; akaenda na kuwapiga Israeli, nao wakauchukua huo mji wa mitende.