Zaburi 83:5 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Maana wanashauriana kwa moyo mmoja, Juu yako wanafanyana agano. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Naam, wanakubaliana kwa moyo mmoja, wanakula kiapo dhidi yako: Biblia Habari Njema - BHND Naam, wanakubaliana kwa moyo mmoja, wanakula kiapo dhidi yako: Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Naam, wanakubaliana kwa moyo mmoja, wanakula kiapo dhidi yako: Neno: Bibilia Takatifu Kwa nia moja wanapanga njama pamoja, wanafanya muungano dhidi yako, Neno: Maandiko Matakatifu Kwa nia moja wanapanga mashauri mabaya pamoja, wanafanya muungano dhidi yako, BIBLIA KISWAHILI Maana wanashauriana kwa moyo mmoja, Juu yako wanafanya agano. |
Akaona haitoshi kumtia mikono Mordekai peke yake; maana wamemjulisha kabila lake Mordekai; kwa hiyo Hamani alitaka kuwaangamiza Wayahudi wote waliokuwa wakikaa katika ufalme wote mzima wa Ahasuero, yaani, watu wake Mordekai.
Wafalme wa dunia wanajipanga, Na wakuu wanafanya shauri pamoja, Juu ya BWANA, Na juu ya masihi wake,
Walisema mioyoni mwao, Na tuwaangamize kabisa; Mahali penye mikutano ya Mungu Wamepachoma moto katika nchi pia.
Kisha watu wa nyumba ya Daudi wakaambiwa kwamba Shamu wamefanya mapatano na Efraimu. Na moyo wake ukataharuki, na moyo wa watu wake, kama miti ya mwituni itikiswavyo na upepo.
Je! Hufikiri neno hili walilolisema watu hawa, wakinena, Jamaa zile mbili alizozichagua BWANA amezitupilia mbali? Hivyo ndivyo wanavyowadharau watu wangu, ili wasiwe taifa tena mbele yao.
Bwana MUNGU asema hivi; Kwa kuwa Wafilisti wametenda mambo kwa kujilipiza kisasi, nao wamejilipiza kisasi kwa moyo wa ujeuri, ili kupaangamiza kwa uadui wa daima;
Na sasa mataifa mengi wamekusanyika juu yako, wasemao, Na atiwe unajisi; macho yetu na yaone shari ya Sayuni.
Maana Wakanaani na wenyeji wote wa nchi hii watasikia habari hii, nao watatuzingira, na kulifuta jina letu katika nchi. Nawe utafanya nini kwa ajili ya jina lako kuu?
Kisha nikamwona huyo mnyama, na wafalme wa nchi, na majeshi yao, wamekutana kufanya vita na yeye aketiye juu ya farasi yule, tena na majeshi yake.