Kwa sababu ya kunighadhibikia kwako, na kwa sababu kutakabari kwako kumefika masikioni mwangu; kwa sababu hiyo nitatia kulabu yangu puani mwako, na hatamu yangu midomoni mwako, nami nitakurudisha nyuma kwa njia ile ile uliyoijia.
Zaburi 83:2 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Maana adui zako wanafanya ghasia, Nao wakuchukiao wameviinua vichwa vyao. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Tazama! Maadui zako wanafanya ghasia; wanaokuchukia wanainua vichwa kwa kiburi. Biblia Habari Njema - BHND Tazama! Maadui zako wanafanya ghasia; wanaokuchukia wanainua vichwa kwa kiburi. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Tazama! Maadui zako wanafanya ghasia; wanaokuchukia wanainua vichwa kwa kiburi. Neno: Bibilia Takatifu Tazama watesi wako wanafanya fujo, jinsi adui zako wanavyoinua vichwa vyao. Neno: Maandiko Matakatifu Tazama watesi wako wanafanya fujo, jinsi adui zako wanavyoinua vichwa vyao. BIBLIA KISWAHILI Maana adui zako wanafanya ghasia, Nao wakuchukiao wameviinua vichwa vyao. |
Kwa sababu ya kunighadhibikia kwako, na kwa sababu kutakabari kwako kumefika masikioni mwangu; kwa sababu hiyo nitatia kulabu yangu puani mwako, na hatamu yangu midomoni mwako, nami nitakurudisha nyuma kwa njia ile ile uliyoijia.
Aha! Uvumi wa watu wengi! Wanavuma kama uvumi wa bahari; Aha! Ngurumo ya mataifa! Wananguruma kama ngurumo ya maji mengi;
Ni nani uliyemshutumu na kumtukana? Umeinua sauti yako juu ya nani, na kuinua macho yako juu? Juu ya Mtakatifu wa Israeli.
Kwa sababu ya kunighadhibikia kwako, na kwa sababu kutakabari kwako kumefika masikioni mwangu, nitatia kulabu yangu katika pua yako, na hatamu yangu midomoni mwako, nami nitakurudisha kwa njia ile ile uliyoijia.
Nao watapigana nawe; lakini hawatakushinda; maana mimi nipo pamoja nawe, asema BWANA, ili nikuokoe.
Basi Pilato alipoona ya kuwa hafai lolote, bali ghasia inazidi tu, akatwaa maji, akanawa mikono yake mbele ya mkutano, akasema, Mimi sina hatia katika damu ya mtu huyu mwenye haki; yaangalieni haya ninyi wenyewe.
Makutano wote wakaondoka wakawaendea, mahakimu wakawavua nguo zao kwa nguvu, wakatoa amri wapigwe kwa bakora.
Na Wayahudi wakaona wivu, wakajitwalia watu kadhaa miongoni mwa watu ovyo wasio na sifa njema, nao wakakutanisha mkutano, wakafanya ghasia mjini, wakawaendea watu wa nyumba ya Yasoni, wakataka kuwapeleka mbele ya watu wa mji;
Mji wote ukataharuki, watu wakakutanika mbio mbio, wakamkamata Paulo, wakamkokota, wakamtoa hekaluni; mara milango ikafungwa.
Wakamsikiliza mpaka neno lile, wakapaza sauti zao, wakisema, Mwondoe huyu katika nchi, kwa maana haifai aishi.
Ugomvi mkubwa ulipotokea, yule jemadari akahofia Paulo asije akararuliwa nao, akaamuru askari washuke na kumwondoa kwa nguvu mikononi mwao, na kumleta ndani ya ngome.
Ndipo Midiani walishindwa mbele ya wana wa Israeli, wala hawakuinua vichwa vyao tena. Nayo nchi ilipata kuwa na amani muda wa miaka arubaini katika siku za Gideoni.