Wewe mwenyewe utasimama, Na kuirehemu Sayuni, Kwa maana ndio wakati wa kuihurumia, Naam, majira yaliyoamriwa yamewadia.
Zaburi 82:8 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Ee Mungu, usimame, uihukumu nchi, Maana mataifa yote ni yako. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Inuka ee Mungu, uuhukumu ulimwengu; maana mataifa yote ni mali yako. Biblia Habari Njema - BHND Inuka ee Mungu, uuhukumu ulimwengu; maana mataifa yote ni mali yako. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Inuka ee Mungu, uuhukumu ulimwengu; maana mataifa yote ni mali yako. Neno: Bibilia Takatifu Ee Mungu, inuka uihukumu nchi, kwa kuwa mataifa yote ni urithi wako. Neno: Maandiko Matakatifu Ee Mungu, inuka uihukumu nchi, kwa kuwa mataifa yote ni urithi wako. BIBLIA KISWAHILI Ee Mungu, usimame, uihukumu nchi, Maana mataifa yote ni yako. |
Wewe mwenyewe utasimama, Na kuirehemu Sayuni, Kwa maana ndio wakati wa kuihurumia, Naam, majira yaliyoamriwa yamewadia.
Kwa ajili ya kuonewa kwao wanyonge, Kwa ajili ya kuugua kwao wahitaji, Sasa nitasimama, asema BWANA, Nitamweka salama yeye wanayemfyonya.
BWANA uondoke kwa hasira yako; Ujiinue Juu ya ujeuri wa watesi wangu; Uamke kwa ajili yangu; Umeamuru hukumu.
Mbele za BWANA, kwa maana anakuja, Kwa maana anakuja aihukumu nchi. Atauhukumu ulimwengu kwa haki, Na mataifa kwa uaminifu wake.
Amka, amka, jivike nguvu, Ee mkono wa Bwana; Amka kama katika siku zile za kale, Katika vizazi vile vya zamani.
Mtu amchaye Mungu ametoweka, asionekane katika nchi, wala hapana mtu mwenye adili katika wanadamu; wote huotea ili kumwaga damu; kila mtu humwinda ndugu yake kwa wavu.
Lakini mimi, nitamtazamia BWANA; nitamngojea Mungu wa wokovu wangu; Mungu wangu atanisikia.
Basi ningojeeni, asema BWANA, hata siku ile nitakapoondoka kuteka mateka; maana nimeazimia kuwakusanya mataifa, ili nizikutanishe falme, nipate kuwamwagia ghadhabu yangu; naam, ukali wote wa hasira yangu; kwa maana dunia yote itateketezwa kwa moto wa wivu wangu.
Malaika wa saba akapiga baragumu, pakawa na sauti kuu katika mbingu, zikisema, Ufalme wa dunia umekwisha kuwa ufalme wa Bwana wetu na wa Kristo wake, naye atamiliki hata milele na milele.