Zaburi 82:5 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Hawajui wala hawafahamu, hutembea gizani; Misingi yote ya nchi imetikisika. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Lakini nyinyi hamjui wala hamfahamu! Nyinyi mnatembea katika giza la upotovu! Misingi yote ya haki duniani imetikiswa! Biblia Habari Njema - BHND “Lakini nyinyi hamjui wala hamfahamu! Nyinyi mnatembea katika giza la upotovu! Misingi yote ya haki duniani imetikiswa! Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Lakini nyinyi hamjui wala hamfahamu! Nyinyi mnatembea katika giza la upotovu! Misingi yote ya haki duniani imetikiswa! Neno: Bibilia Takatifu “Hawajui lolote, hawaelewi lolote. Wanatembea gizani; misingi yote ya dunia imetikisika. Neno: Maandiko Matakatifu “Hawajui lolote, hawaelewi lolote. Wanatembea gizani; misingi yote ya dunia imetikisika. BIBLIA KISWAHILI Hawajui wala hawafahamu, hutembea gizani; Misingi yote ya nchi imetikisika. |
macho yake mwenye hekima yamo kichwani mwake, lakini mpumbavu huenda gizani; ila hata hivyo nikatambua ya kwamba ni tukio moja la mwisho liwapatalo wote sawasawa.
Zaidi ya hayo, nikaona tena chini ya jua ya kwamba, Mahali pa hukumu upo uovu, Na mahali pa haki upo udhalimu.
Kwa maana shamba la mizabibu la BWANA wa majeshi ndilo nyumba ya Israeli, na watu wa Yuda ni mche wake wa kupendeza; akatumaini kuona hukumu ya haki, na kumbe! Aliona dhuluma; alitumaini kuona haki, na kumbe! Alisikia kilio.
Kwa sababu hiyo hukumu ya haki iko mbali nasi, wala haki haitufikii; twatazamia nuru, na kumbe! Latokea giza; twatazamia mwanga, lakini twaenda katika giza kuu.
Nikasema, Tafadhali sikieni, enyi vichwa vya Yakobo, mnaoitawala nyumba ya Israeli. Je! Haiwapasi ninyi kujua hukumu?
Basi Yesu akawaambia, Nuru ingaliko pamoja nanyi muda kidogo. Nendeni maadamu mnayo nuru hiyo, giza lisije likawaweza; maana aendaye gizani hajui aendako.
Na hii ndiyo hukumu; ya kuwa nuru imekuja ulimwenguni, na watu wakapenda giza kuliko nuru; kwa maana matendo yao yalikuwa maovu.
Na kama walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao, Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa, wayafanye yasiyowapasa.
Lakini msingi wa Mungu ulio imara umesimama, wenye mhuri huu, Bwana awajua walio wake. Na tena, Kila aliitaye jina la Bwana na auache uovu.
Bali yeye amchukiaye ndugu yake, yuko katika giza, tena anakwenda katika giza, wala hajui aendako, kwa sababu giza imempofusha macho.