Hao ndio waliokuwa wafinyanzi, na wenyeji wa Netaimu na Gedera; ndipo walipokaa pamoja na mfalme ili kufanya kazi yake.
Zaburi 81:6 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Nimeutua mzigo begani mwake; Mikono yake nikaiondolea kazi nzito. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Mimi nilikutua mizigo yako mabegani, nilikuondolea matofali uliyochukua mikononi. Biblia Habari Njema - BHND “Mimi nilikutua mizigo yako mabegani, nilikuondolea matofali uliyochukua mikononi. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Mimi nilikutua mizigo yako mabegani, nilikuondolea matofali uliyochukua mikononi. Neno: Bibilia Takatifu Asema, “Nimeondoa mzigo mabegani mwao; mikono yao iliwekwa huru kutoka kwa kikapu. Neno: Maandiko Matakatifu Asema, “Nimeondoa mzigo mabegani mwao; mikono yao iliwekwa huru kutoka kwenye kikapu. BIBLIA KISWAHILI Nimeutua mzigo begani mwake; Mikono yake nikaiondolea kazi nzito. |
Hao ndio waliokuwa wafinyanzi, na wenyeji wa Netaimu na Gedera; ndipo walipokaa pamoja na mfalme ili kufanya kazi yake.
Huko ndiko wapandako kabila, makabila ya BWANA; Kama ulivyowaamuru Waisraeli, Walishukuru jina la BWANA.
Kwa nini kulala mazizini arukapo hua, Mbawa zake ziking'aa kama fedha Na manyoya yake kama dhahabu?
wakafanya maisha yao kuwa machungu kwa kazi ngumu; kazi ya chokaa na ya matofali, na kila namna ya kazi ya mashamba; kwa kazi zao zote walizowatumikisha kwa ukali.
Basi waambie wana wa Israeli, Mimi ni BWANA nami nitawatoa ninyi mtoke chini ya ukandamizaji wa Wamisri, nami nitawaokoa kutoka utumwa wao, nami nitawakomboa kwa mkono ulionyoshwa, na kwa hukumu kubwa;
Tena itakuwa katika siku hiyo mzigo wake utaondoka begani mwako, na nira yake shingoni mwako, nayo nira itaharibiwa, kwa sababu ya kutiwa mafuta.
Kwa maana umeivunja nira ya mzigo wake, na gongo la bega lake, na fimbo yake yeye aliyemwonea, kama katika siku ya Midiani.
Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu;