Zaburi 81:15 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Wamchukiao BWANA wangenyenyekea mbele zake, Na maangamizi yao yangedumu milele. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wanichukiao wangenipigia magoti kwa hofu, na adhabu yao ingekuwa ya milele. Biblia Habari Njema - BHND Wanichukiao wangenipigia magoti kwa hofu, na adhabu yao ingekuwa ya milele. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wanichukiao wangenipigia magoti kwa hofu, na adhabu yao ingekuwa ya milele. Neno: Bibilia Takatifu Wale wanaomchukia Mwenyezi Mungu wangejikunyata mbele zake, na adhabu yao ingedumu milele. Neno: Maandiko Matakatifu Wale wanaomchukia bwana wangalinyenyekea mbele zake, na adhabu yao ingedumu milele. BIBLIA KISWAHILI Wamchukiao BWANA wangenyenyekea mbele zake, Na maangamizi yao yangedumu milele. |
Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, BWANA, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao,
Hawatajenga, kisha akakaa mtu mwingine ndani yake; hawatapanda, kisha akala mtu mwingine; maana kama siku za mti ndivyo zitakavyokuwa siku za watu wangu, na wateule wangu wataifurahia kazi ya mikono yao muda wa siku nyingi.
wenye kusingizia, wenye kumchukia Mungu, wenye jeuri, wenye kutakabari, wenye majivuno, wenye kutunga mabaya, wasiowatii wazazi wao,
Kwa kuwa ile nia ya mwili ni uadui juu ya Mungu, kwa maana haitii sheria ya Mungu, wala haiwezi kuitii.
naye huwalipa wamchukiao mbele ya uso wao, kuwaangamiza. Hatakuwa mlegevu kwake yeye amchukiaye, atamlipa mbele ya uso wake.