Zaburi 81:14 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Ningewadhili adui zao kwa upesi, Na juu ya watesi wao ningegeuza mkono wangu; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Ningewashinda maadui zao haraka; ningenyosha mkono dhidi ya wadhalimu wao. Biblia Habari Njema - BHND Ningewashinda maadui zao haraka; ningenyosha mkono dhidi ya wadhalimu wao. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Ningewashinda maadui zao haraka; ningenyosha mkono dhidi ya wadhalimu wao. Neno: Bibilia Takatifu ningewatiisha adui zao kwa haraka, na kuugeuza mkono wangu dhidi ya watesi wao! Neno: Maandiko Matakatifu ningaliwatiisha adui zao kwa haraka, na kuugeuza mkono wangu dhidi ya watesi wao! BIBLIA KISWAHILI Ningewadhili adui zao kwa upesi, Na juu ya watesi wao ningegeuza mkono wangu; |
Laiti ungalisikiliza amri zangu! Ndipo amani yako ingalikuwa kama mto wa maji, na haki yako kama mawimbi ya bahari;
Nami nitamkatilia mbali mwenyeji katika Ashdodi; na yeye aishikaye fimbo ya enzi katika Ashkeloni; nami nitaugeuza mkono wangu uwe juu ya Ekroni; na mabaki ya Wafilisti wataangamia, asema Bwana MUNGU.
Amka, Ee upanga, juu ya mchungaji wangu, na juu ya mtu aliye mwenzangu, asema BWANA wa majeshi; mpige mchungaji, nao kondoo watatawanyika; nami nitaugeuza mkono wangu juu ya wadogo.
Ndipo Mwamaleki, na Mkanaani waliokaa huko mlimani, wakateremka, wakawapiga na kuwaangusha, hadi wakafika Horma.
Lakini msimwasi BWANA, wala msiwaogope wale wenyeji wa nchi, maana wao ni chakula kwetu; kinga iliyokuwa juu yao imeondolewa, naye BWANA yuko pamoja nasi; msiwaogope.
Na sasa, Israeli, BWANA, Mungu wako, anataka nini kwako, ila umche BWANA, Mungu wako, na kwenda katika njia zake zote, na kumpenda, na kumtumikia BWANA, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote;
jueni hakika ya kuwa BWANA, Mungu wenu, hatawafukuza tena mataifa haya mbele ya macho yenu, bali watakuwa mtego kwenu na tanzi, na mjeledi mbavuni mwenu, na miiba machoni mwenu, hadi mtakapoangamia na kutoka katika nchi hii njema, ambayo BWANA, Mungu wenu, amewapa ninyi.