Akasema, Nenda, ukaazime vyombo huko nje kwa jirani zako wote, vyombo vitupu; wala usiazime vichache.
Zaburi 81:11 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Lakini watu wangu hawakuisikiliza sauti yangu, Wala Israeli hawakunitaka. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema “Lakini watu wangu hawakunisikiliza; Israeli hakunitaka kabisa. Biblia Habari Njema - BHND “Lakini watu wangu hawakunisikiliza; Israeli hakunitaka kabisa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza “Lakini watu wangu hawakunisikiliza; Israeli hakunitaka kabisa. Neno: Bibilia Takatifu “Lakini watu wangu hawakunisikiliza; Israeli hakunitii. Neno: Maandiko Matakatifu “Lakini watu wangu hawakutaka kunisikiliza; Israeli hakutaka kunitii. BIBLIA KISWAHILI Lakini watu wangu hawakuisikiliza sauti yangu, Wala Israeli hawakunitaka. |
Akasema, Nenda, ukaazime vyombo huko nje kwa jirani zako wote, vyombo vitupu; wala usiazime vichache.
Musa na Haruni wakawaambia wana wote wa Israeli, Jioni ndipo mtakapojua ya kuwa BWANA amewaleta kutoka nchi ya Misri;
Hata watu walipoona ya kuwa Musa amekawia kushuka katika mlima, wakakusanyana wakamwendea Haruni, wakamwambia, Haya! Katufanyizie miungu itakayokwenda mbele yetu, kwa maana Musa huyo aliyetutoa katika nchi ya Misri hatujui yaliyompata.
Basi waambie wana wa Israeli, Mimi ni BWANA nami nitawatoa ninyi mtoke chini ya ukandamizaji wa Wamisri, nami nitawaokoa kutoka utumwa wao, nami nitawakomboa kwa mkono ulionyoshwa, na kwa hukumu kubwa;
Kwa hiyo, angalia, siku zinakuja, asema BWANA, ambapo hawatasema tena, Aishivyo BWANA, aliyewaleta wana wa Israeli toka nchi ya Misri;
Lakini hao walikataa kusikiliza, wakageuza bega lao, wakaziba masikio yao ili wasisikie.
Lakini Yeshuruni alinenepa, akapiga teke; Umenenepa, umekuwa mnene, umewanda; Ndipo akamwacha Mungu aliyemfanya, Akamdharau Mwamba wa wokovu wake.
Mwaonaje? Haikumpasa adhabu iliyo kubwa zaidi mtu yule aliyemkanyaga Mwana wa Mungu, na kuihesabu damu ya agano aliyotakaswa kwayo kuwa ni kitu ovyo, na kumfanyia jeuri Roho wa neema?