Tena nitawaagizia mahali watu wangu Israeli, nami nitawapanda, wapate kukaa mahali pao wenyewe, wasiondolewe tena; wala wana wa uovu hawatawatesa tena, kama hapo kwanza;
Zaburi 80:9 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Ulitengeneza nafasi mbele yake, Nao ukatia mizizi sana ukaijaza nchi. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Uliupalilia upate kukua, nao ukatoa mizizi na kuenea kote nchini. Biblia Habari Njema - BHND Uliupalilia upate kukua, nao ukatoa mizizi na kuenea kote nchini. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Uliupalilia upate kukua, nao ukatoa mizizi na kuenea kote nchini. Neno: Bibilia Takatifu Uliandaa shamba kwa ajili yake, mizizi ikawa imara, ukajaza nchi. Neno: Maandiko Matakatifu Uliandaa shamba kwa ajili yake, mizizi ikawa imara, ukajaza nchi. BIBLIA KISWAHILI Ulitengeneza nafasi mbele yake, Nao ukatia mizizi sana ukaijaza nchi. |
Tena nitawaagizia mahali watu wangu Israeli, nami nitawapanda, wapate kukaa mahali pao wenyewe, wasiondolewe tena; wala wana wa uovu hawatawatesa tena, kama hapo kwanza;
Yuda na Israeli walikuwa wengi kama mchanga wa pwani kwa wingi, wakila, na kunywa, na kufurahi.
Yuda na Israeli wakakaa salama, kila mtu chini ya mzabibu wake na chini ya mtini wake, tokea Dani mpaka Beer-sheba, siku zote za Sulemani.
Naye Yoabu akamtolea Daudi jumla ya hesabu ya watu. Na hao wote wa Israeli walikuwa watu milioni moja na laki moja, wenye kufuta panga; na wa Yuda watu elfu mia nne sabini (470,000), wenye kufuta panga.
Maana hawakuitwaa nchi kwa upanga wao, Wala hawakupata ushindi kwa mkono wao; Bali mkono wako wa kulia, naam, mkono wako, Na nuru ya uso wako, kwa kuwa ulipendezwa nao.
Siku zijazo Yakobo atatia mizizi; Israeli atatoa maua na kuchipuka; Nao watajaza uso wa ulimwengu matunda.
Na mabaki yaliyookoka, yaliyobakia ya nyumba ya Yuda, yatatia mizizi chini, na kuzaa matunda juu.
Akachimba handaki kulizunguka pande zote, Akatoa mawe yake, Akapanda ndani yake mzabibu ulio mzuri, Akajenga mnara katikati yake, Akachimba shinikizo ndani yake; Akatumaini ya kuwa utazaa zabibu, Nao ukazaa zabibumwitu.
Umewapanda, naam, wametia mizizi, wanakua, naam, wanazaa matunda; katika vinywa vyao u karibu, bali katika mioyo yao u mbali.
Nami nilikuwa nimekupanda, mzabibu mwema sana, mbegu nzuri kabisa; umegeukaje, basi, kuwa mche usiofaa wa mzabibumwitu machoni pangu?
Nikatuma nyigu mbele yenu, waliowafukuza mbele yenu hao wafalme wawili wa Waamori, si kwa upanga wako, wala kwa upinde wako.