Lakini Sanbalati, Mhoroni, na Tobia, mtumishi wake, Mwamoni, na Geshemu, Mwarabu, walitucheka, wakatudharau, wakasema, Ni nini neno hili mnalofanya? Je! Ninyi mtaasi juu ya mfalme?
Zaburi 80:7 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Ee Mungu wa majeshi, uturudishe, Uangaze uso wako nasi tutaokoka. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Ee Mungu wa majeshi, uturekebishe, utuangalie kwa wema, nasi tutaokoka. Biblia Habari Njema - BHND Ee Mungu wa majeshi, uturekebishe, utuangalie kwa wema, nasi tutaokoka. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Ee Mungu wa majeshi, uturekebishe, utuangalie kwa wema, nasi tutaokoka. Neno: Bibilia Takatifu Ee Mungu wa majeshi ya mbinguni, uturejeshe; utuangazie uso wako, nasi tuweze kuokolewa. Neno: Maandiko Matakatifu Ee Mungu Mwenye Nguvu Zote, uturejeshe; utuangazie uso wako, nasi tuweze kuokolewa. BIBLIA KISWAHILI Ee Mungu wa majeshi, uturudishe, Uangaze uso wako nasi tutaokoka. |
Lakini Sanbalati, Mhoroni, na Tobia, mtumishi wake, Mwamoni, na Geshemu, Mwarabu, walitucheka, wakatudharau, wakasema, Ni nini neno hili mnalofanya? Je! Ninyi mtaasi juu ya mfalme?
Kwa maana Bwana MUNGU, Mtakatifu wa Israeli, asema hivi, Kwa kurudi na kustarehe mtaokolewa; nguvu zenu zitakuwa katika kutulia na kutumaini; lakini hamkukubali.
Wewe wamlaki yeye afurahiaye yaliyo haki na kuyatenda, watu wale wakukumbukao katika njia zako; tazama, ulikuwa na hasira, nasi tulitenda dhambi; tumekuwa katika dhambi kwa muda mrefu, nasi Je! Tutaokolewa?
Ee Yerusalemu, jioshe moyo wako usiwe na uovu, upate kuokoka. Mawazo yako mabaya yatakaa ndani yako hata lini?
ili wakitazama watazame, wasione; Na wakisikia wasikie, wasielewe; Wasije wakaongoka, na kusamehewa.