Siku ile BWANA akafanya agano na Abramu, akasema, Uzao wako nimewapa nchi hii, kutoka mto wa Misri mpaka huo mto mkubwa, mto Frati,
Zaburi 80:11 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Nao uliyaeneza matawi yake hadi baharini, Na vichipukizi vyake hadi kunako Mto. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Matawi yake yalienea mpaka baharini; machipukizi yake mpaka kando ya mto Eufrate. Biblia Habari Njema - BHND Matawi yake yalienea mpaka baharini; machipukizi yake mpaka kando ya mto Eufrate. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Matawi yake yalienea mpaka baharini; machipukizi yake mpaka kando ya mto Eufrate. Neno: Bibilia Takatifu Matawi yake yalienea hadi Baharini, machipukizi yake hadi kwenye Mto. Neno: Maandiko Matakatifu Matawi yake yalienea mpaka Baharini, machipukizi yake mpaka kwenye Mto. BIBLIA KISWAHILI Nao uliyaeneza matawi yake hadi baharini, Na vichipukizi vyake hadi kunako Mto. |
Siku ile BWANA akafanya agano na Abramu, akasema, Uzao wako nimewapa nchi hii, kutoka mto wa Misri mpaka huo mto mkubwa, mto Frati,
Sulemani akatawala juu ya falme zote, toka Mto mpaka nchi ya Wafilisti, na hata mpaka wa Misri; walimletea tunu, na kumtumikia Sulemani siku zote za maisha yake.
Kwani alikuwa akitawala nchi yote upande huu wa Mto, toka Tifsa mpaka Gaza, juu ya wafalme wote wa upande huu wa Mto; naye alikuwa na amani pande zake zote.
Tena Daudi akampiga Hadadezeri, mfalme wa Soba, mpaka Hamathi, alipokwenda kujisimamishia mnara wa ukumbusho kwenye mto wa Frati.
Nami nitakuwekea mpaka wako tangu Bahari ya Shamu hadi bahari ya Wafilisti, tena tangu jangwani hata huo Mto; kwa kuwa nitawatia wenyeji wa nchi mkononi mwako; nawe utawafukuza mbele yako.