Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila kiumbe kitambaacho nchini.
Zaburi 8:7 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Kondoo, na ng'ombe wote pia; Naam, na wanyama wa porini; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Kondoo, ng'ombe, na wanyama wa porini; Biblia Habari Njema - BHND Kondoo, ng'ombe, na wanyama wa porini; Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza kondoo, ng'ombe, na wanyama wa porini; Neno: Bibilia Takatifu Mifugo na makundi yote pia, naam, na wanyama wa kondeni, Neno: Maandiko Matakatifu Mifugo na makundi yote pia, naam, na wanyama wa kondeni, BIBLIA KISWAHILI Kondoo, na ng'ombe wote pia; Naam, na wanyama wa porini; |
Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila kiumbe kitambaacho nchini.
Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuimiliki; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi.
Adamu akawapa majina yao kila mnyama wa kufugwa, na ndege wa angani, na kila mnyama wa mwituni; lakini hakuonekana wa kumsaidia Adamu aliyefanana naye.