BWANA Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa kiumbe hai.
Zaburi 8:5 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Umemfanya mdogo kuliko Mungu; Umemvika taji la utukufu na heshima; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Umemfanya awe karibu kama Mungu, umemvika fahari na heshima. Biblia Habari Njema - BHND Umemfanya awe karibu kama Mungu, umemvika fahari na heshima. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Umemfanya awe karibu kama Mungu, umemvika fahari na heshima. Neno: Bibilia Takatifu Umemfanya chini kidogo kuliko viumbe wa mbinguni, ukamvika taji la utukufu na heshima. Neno: Maandiko Matakatifu Umemfanya chini kidogo kuliko viumbe wa mbinguni, ukamvika taji ya utukufu na heshima. BIBLIA KISWAHILI Umemfanya mdogo kuliko Mungu; Umemvika taji la utukufu na heshima; |
BWANA Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa kiumbe hai.
Ndipo Absalomu akatuma Yoabu aitwe, amtume kwa mfalme, lakini yeye akakataa kumjia; akatuma tena mara ya pili, lakini akakataa kuja.
Mhimidini BWANA, enyi malaika zake, Ninyi mlio hodari, mtendao neno lake, Mkiisikiliza sauti ya neno lake.
Kiti chako cha enzi, Mungu, ni cha milele na milele, Fimbo ya ufalme wako ni fimbo ya adili.
juu sana kuliko ufalme wote, na mamlaka, na nguvu, na utawala, na kila jina litajwalo, wala si ulimwenguni humu tu, bali katika ule ujao pia;
Umemfanya mdogo kwa muda kuliko malaika, Umemvika taji la utukufu na heshima, Umemtawaza juu ya kazi za mikono yako;
ila twamwona yeye aliyefanywa mdogo kwa muda kuliko malaika, yaani, Yesu, kwa sababu ya maumivu ya mauti, amevikwa taji la utukufu na heshima, ili kwa neema ya Mungu aionje mauti kwa ajili ya kila mtu.