Zaburi 79:8 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Usikumbuke juu yetu maovu ya baba zetu, Rehema zako zije kutulaki haraka, Kwa maana tumeteseka sana. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Usituadhibu kwa sababu ya makosa ya wazee wetu. Huruma yako itujie haraka, maana tumekandamizwa mno! Biblia Habari Njema - BHND Usituadhibu kwa sababu ya makosa ya wazee wetu. Huruma yako itujie haraka, maana tumekandamizwa mno! Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Usituadhibu kwa sababu ya makosa ya wazee wetu. Huruma yako itujie haraka, maana tumekandamizwa mno! Neno: Bibilia Takatifu Usituhesabie dhambi za baba zetu, huruma yako na itujie hima, kwa maana tu wahitaji mno. Neno: Maandiko Matakatifu Usituhesabie dhambi za baba zetu, huruma yako na itujie hima, kwa maana tu wahitaji mno. BIBLIA KISWAHILI Usikumbuke juu yetu maovu ya baba zetu, Rehema zako zije kutulaki haraka, Kwa maana tumeteseka sana. |
Akamwambia Eliya, Nina nini nawe, Ee mtu wa Mungu? Je! Umenijia ili dhambi yangu ikumbukwe, ukamwue mwanangu?
Mara nyingi aliwaponya, Bali walikuwa wakimwasi kwa mashauri yao, Wakawa dhalili kwa uovu wao.
Ukisikilize kilio changu, Kwa maana nimedhilika sana. Uniponye kutoka kwa wanaonifuatia, Kwa maana wao ni hodari kuliko mimi.
Usiyakumbuke makosa ya ujana wangu, Wala maasi yangu. Unikumbuke kwa kadiri ya fadhili zako, Ee BWANA kwa ajili ya wema wako.
Basi sasa uende ukawaongoze watu hawa mpaka mahali pale ambapo nimekwambia habari zake; tazama, malaika wangu atakutangulia; pamoja na hayo siku nitakayowajia nitawapatiliza kwa ajili ya dhambi yao.
Ee BWANA, usione hasira nyingi, wala usiukumbuke uovu siku zote; tazama, angalia, twakusihi, sisi sote tu watu wako.
Akaniambia, Mwanadamu, nakutuma kwa wana wa Israeli, kwa mataifa wanaoasi, walioniasi mimi; wao na baba zao wameasi juu yangu, naam, hata hivi leo.
Ee Bwana sawasawa na haki yako yote, nakusihi, hasira yako na ghadhabu yako zigeuzwe na kuuacha mji wako Yerusalemu, mlima wako mtakatifu; maana kwa sababu ya dhambi zetu, na maovu ya baba zetu, Yerusalemu na watu wako wamepata kulaumiwa na watu wote wanaotuzunguka.
Kwa habari za dhabihu za matoleo yangu, hutoa dhabihu ya nyama na kuila; lakini BWANA hawakubali; sasa ataukumbuka uovu wao, na kuwapatiliza dhambi zao; watarudi kwenda Misri.
Wamejiharibu mno, kama katika siku za Gibea; ataukumbuka uovu wao, atazilipiza dhambi zao.