ili kulitimiza neno la BWANA kwa kinywa cha Yeremia, hata nchi itakapofurahia sabato zake; kwa maana siku zote ilipokaa ukiwa ilishika sabato, kutimiza miaka sabini.
Zaburi 79:7 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Kwa maana wamemla Yakobo, Na makao yake wameyaharibu. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Maana wamemmeza Yakobo, taifa lako, wameteketeza kabisa makao yake. Biblia Habari Njema - BHND Maana wamemmeza Yakobo, taifa lako, wameteketeza kabisa makao yake. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Maana wamemmeza Yakobo, taifa lako, wameteketeza kabisa makao yake. Neno: Bibilia Takatifu kwa maana wamemrarua Yakobo na kuharibu nchi ya makao yake. Neno: Maandiko Matakatifu kwa maana wamemrarua Yakobo na kuharibu nchi ya makao yake. BIBLIA KISWAHILI Kwa maana wamemla Yakobo, Na makao yake wameyaharibu. |
ili kulitimiza neno la BWANA kwa kinywa cha Yeremia, hata nchi itakapofurahia sabato zake; kwa maana siku zote ilipokaa ukiwa ilishika sabato, kutimiza miaka sabini.
Ee BWANA, usione hasira nyingi, wala usiukumbuke uovu siku zote; tazama, angalia, twakusihi, sisi sote tu watu wako.
Waashuri upande wa mbele, na Wafilisti upande wa nyuma, nao watamla Israeli kwa kinywa kilicho wazi. Pamoja na hayo yote hasira yake haikugeukia mbali, lakini mkono wake umenyoshwa hata sasa.
Watu wote waliowaona wamewala; na adui zao walisema, Sisi hatuna hatia, kwa kuwa hao wametenda dhambi juu ya BWANA, aliye kao la haki, yaani, BWANA, tumaini la baba zao.
Nami ninayakasirikia sana mataifa yanayostarehe; kwa maana mimi nilikuwa nimekasirika kidogo tu, nao wakayazidisha maafa.