BWANA akamwambia, Kwa sababu hiyo yeyote atakayemwua Kaini atalipizwa kisasi mara saba. BWANA akamtia Kaini alama, mtu amwonaye asije akampiga.
Zaburi 79:12 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Uwalipe jirani zetu mara saba vifuani mwao Laumu zao walizokulaumu, Ee Bwana. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mataifa hayo yaliyokudharau, ee Bwana, yalipizwe mara saba! Biblia Habari Njema - BHND Mataifa hayo yaliyokudharau, ee Bwana, yalipizwe mara saba! Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mataifa hayo yaliyokudharau, ee Bwana, yalipizwe mara saba! Neno: Bibilia Takatifu Walipize majirani zetu mara saba aibu walizovurumisha kwako, Ee Bwana. Neno: Maandiko Matakatifu Walipize jirani zetu mara saba vifuani mwao aibu walizovurumisha juu yako, Ee bwana. BIBLIA KISWAHILI Uwalipe jirani zetu mara saba vifuani mwao Laumu zao walizokulaumu, Ee Bwana. |
BWANA akamwambia, Kwa sababu hiyo yeyote atakayemwua Kaini atalipizwa kisasi mara saba. BWANA akamtia Kaini alama, mtu amwonaye asije akampiga.
wewe uwarehemuye watu elfu nyingi, uwalipaye baba za watu uovu wao vifuani mwa watoto wao baada yao; Mungu aliye mkuu, aliye hodari, BWANA wa majeshi ndilo jina lake;
Nawe utajua ya kuwa mimi, BWANA, nimeyasikia matusi yako yote, uliyoyanena juu ya milima ya Israeli, ukisema, Wamefanyika ukiwa, wametiwa katika mikono yetu tuwale.
basi Bwana MUNGU asema hivi; Nimeinua mkono wangu, kusema, Hakika, mataifa walio karibu nanyi pande zote, nao watatukanwa.
Nanyi ikiwa mnaenda kinyume changu, wala hamtaki kunisikiza; nitaleta mapigo mara saba zaidi juu yenu, kama dhambi zenu zilivyo.
ndipo nami nitawaendea kinyume katika ghadhabu yangu; nami nitawaadhibu mara saba kwa dhambi zenu.
Wapeni watu vitu, nanyi mtapewa; kipimo cha kujaa na kushindiliwa, na kusukwasukwa hata kumwagika, ndicho watu watakachowapa vifuani mwenu. Kwa kuwa kipimo kile kile mpimacho ndicho mtakachopimiwa.