Walikuwa wenye kupinda upinde, nao walikuwa hodari wa kutumia mkono wa kulia na wa kushoto, kwa kutupa mawe ya teo, na kwa kupiga mishale ya upinde; walikuwa wa nduguze Sauli, wa Benyamini.
Zaburi 78:9 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Wale Waefraimu, wenye silaha, wapiga upinde, Walirudi nyuma siku ya vita. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Watu wa Efraimu, pinde na mishale mkononi, walirudi nyuma, wakakimbia siku ile ya vita. Biblia Habari Njema - BHND Watu wa Efraimu, pinde na mishale mkononi, walirudi nyuma, wakakimbia siku ile ya vita. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Watu wa Efraimu, pinde na mishale mkononi, walirudi nyuma, wakakimbia siku ile ya vita. Neno: Bibilia Takatifu Watu wa Efraimu, ingawa walijifunga pinde, walikimbia siku ya vita. Neno: Maandiko Matakatifu Watu wa Efraimu, ingawa walijifunga pinde, walikimbia siku ya vita. BIBLIA KISWAHILI Wale Waefraimu, wenye silaha, wapiga upinde, Walirudi nyuma siku ya vita. |
Walikuwa wenye kupinda upinde, nao walikuwa hodari wa kutumia mkono wa kulia na wa kushoto, kwa kutupa mawe ya teo, na kwa kupiga mishale ya upinde; walikuwa wa nduguze Sauli, wa Benyamini.
Nao watu wa Israeli walipogeuka katika ile vita, Benyamini naye akaanza kupiga na kuwaua watu wa Israeli kama watu thelathini; kwani walisema, Hakika yetu wamepigwa mbele yetu, vile vile kama katika ile vita ya kwanza.
Naye Gaali mwana wa Ebedi akasema, Abimeleki ni nani, na sisi wa Shekemu ni nani, hata tukamtumikie yeye? Je, huyu mwana wa Yerubaali na Zebuli afisa wake hawakuwatumikia watu wa Hamori babaye Shekemu? Basi, kwa nini tumutumikie?
Basi Wafilisti wakapigana na Israeli; nao watu wa Israeli wakawakimbia Wafilisti, wakauawa katika mlima wa Gilboa.
Wafilisti wakapigana nao, Israeli wakapigwa, wakakimbia kila mtu hemani kwake; wakauawa watu wengi sana; maana katika Israeli walianguka watu elfu thelathini walioenda vitani kwa miguu.