basi, sasa, fanyeni hayo; kwa maana BWANA amemtaja Daudi, akisema, kwa mkono wa mtumishi wangu, Daudi, nitawaokoa watu wangu Israeli katika mikono ya Wafilisti, na katika mikono ya adui zao wote.
Zaburi 78:70 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Akamchagua Daudi, mtumishi wake, Akamwondoa katika mazizi ya kondoo. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Alimchagua Daudi, mtumishi wake, akamtoa katika kazi ya kuchunga kondoo. Biblia Habari Njema - BHND Alimchagua Daudi, mtumishi wake, akamtoa katika kazi ya kuchunga kondoo. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Alimchagua Daudi, mtumishi wake, akamtoa katika kazi ya kuchunga kondoo. Neno: Bibilia Takatifu Akamchagua Daudi mtumishi wake na kumtoa kwenye mazizi ya kondoo. Neno: Maandiko Matakatifu Akamchagua Daudi mtumishi wake na kumtoa kwenye mazizi ya kondoo. BIBLIA KISWAHILI Akamchagua Daudi, mtumishi wake, Akamwondoa katika mazizi ya kondoo. |
basi, sasa, fanyeni hayo; kwa maana BWANA amemtaja Daudi, akisema, kwa mkono wa mtumishi wangu, Daudi, nitawaokoa watu wangu Israeli katika mikono ya Wafilisti, na katika mikono ya adui zao wote.
Daudi akamwambia Mikali, Ilikuwa mbele za BWANA, aliyenichagua mimi juu ya baba yako, na juu ya nyumba yake, ili kuniweka niwe mkuu juu ya watu wa BWANA, juu ya Israeli; kwa hiyo mimi nitacheza mbele za BWANA.
Basi, sasa, mwambie mtumishi wangu, Daudi, maneno haya, BWANA wa majeshi asema hivi, Nilikutwaa katika zizi la kondoo, katika kuwaandama kondoo, ili uwe mkuu juu ya watu wangu, juu ya Israeli;
Tokea siku ile nilipowatoa watu wangu Israeli katika Misri, sikuchagua mji wowote katika kabila zote za Israeli ili kujenga nyumba, jina langu liwe hapo; lakini nilimchagua Daudi awe juu ya watu wangu Israeli.
Basi huyo Musa alikuwa akilichunga kundi la Yethro mkwewe, kuhani wa Midiani; akaliongoza kundi nyuma ya jangwa, akafika mpaka mlima wa Mungu, hata Horebu.
Haya, basi, nitakutuma sasa kwa Farao, ili upate kuwatoa watu wangu, hao wana wa Israeli, katika Misri.
Na alipokwisha kumwondoa huyo, akamwinua Daudi awe mfalme wao ambaye alimshuhudia, akisema, Nimemwona Daudi, mwana wa Yese, mtu anayeupendeza moyo wangu, atakayefanya mapenzi yangu yote.