Zaburi 78:62 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Akawatoa watu wake wapigwe kwa upanga; Akaughadhibikia urithi wake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Aliwakasirikia watu wake mwenyewe; akawatoa waangamizwe kwa upanga. Biblia Habari Njema - BHND Aliwakasirikia watu wake mwenyewe; akawatoa waangamizwe kwa upanga. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Aliwakasirikia watu wake mwenyewe; akawatoa waangamizwe kwa upanga. Neno: Bibilia Takatifu Aliachia watu wake wauawe kwa upanga, akaukasirikia sana urithi wake. Neno: Maandiko Matakatifu Aliachia watu wake wauawe kwa upanga, akaukasirikia sana urithi wake. BIBLIA KISWAHILI Akawatoa watu wake wapigwe kwa upanga; Akaughadhibikia urithi wake. |
Ee BWANA, usione hasira nyingi, wala usiukumbuke uovu siku zote; tazama, angalia, twakusihi, sisi sote tu watu wako.
Wamepanda ngano, lakini watavuna miiba; wamejiumiza nafsi zao, lakini hawatakuwa na faida; naam, tahayarini kwa ajili ya matunda yenu, kwa sababu ya hasira kali ya BWANA.
Nimeiacha nyumba yangu, nimeutupa urithi wangu; nimemtia mpenzi wangu katika mikono ya adui zake.
Nao Wafilisti wakajipanga juu ya Israeli; na walipopigana, Waisraeli wakapigwa na Wafilisti; waliowaua karibu elfu nne katika uwanja wa vita.