Sasa, Ee BWANA, Mungu, uondoke, uende kwenye raha yako, wewe na sanduku la nguvu zako; makuhani wako, Ee BWANA, Mungu, wavikwe wokovu, watakatifu wako na washangilie mema.
Zaburi 78:61 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Akaziacha nguvu zake kutekwa, Na fahari yake mkononi mwa mtesi. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Aliiacha ishara ya nguvu yake itekwe, utukufu wake utiwe mikononi mwa maadui. Biblia Habari Njema - BHND Aliiacha ishara ya nguvu yake itekwe, utukufu wake utiwe mikononi mwa maadui. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Aliiacha ishara ya nguvu yake itekwe, utukufu wake utiwe mikononi mwa maadui. Neno: Bibilia Takatifu Akalipeleka Sanduku la nguvu zake utumwani, utukufu wake mikononi mwa adui. Neno: Maandiko Matakatifu Akalipeleka Sanduku la nguvu zake utumwani, utukufu wake mikononi mwa adui. BIBLIA KISWAHILI Akaziacha nguvu zake kutekwa, Na fahari yake mkononi mwa mtesi. |
Sasa, Ee BWANA, Mungu, uondoke, uende kwenye raha yako, wewe na sanduku la nguvu zako; makuhani wako, Ee BWANA, Mungu, wavikwe wokovu, watakatifu wako na washangilie mema.
Inueni vichwa vyenu, enyi malango, Inukeni, enyi malango ya milele, Mfalme wa utukufu apate kuingia.
Ndipo lile wingu likaifunikiza hema ya kukutania, na huo utukufu wa BWANA ukaijaza maskani.
Kisha wana wa Dani wakajisimamishia hiyo sanamu ya kuchonga; na Yonathani mwana wa Gershomu, mwana wa Musa, yeye na wanawe walikuwa ni makuhani katika kabila la Wadani hadi siku nchi hiyo ilipochukuliwa mateka.
Yeye aliyeleta habari akajibu, akasema, Israeli wamekimbia mbele ya Wafilisti, tena watu wengi sana wameuawa, hata na wana wako wawili, Hofni na Finehasi, wamekufa pia, na sanduku la Mungu limetwaliwa.
Akamwita mtoto, Ikabodi, akisema, Huo utukufu umeondoka katika Israeli; kwa sababu sanduku la Mungu lilikuwa limetwaliwa, na kwa sababu ya mkwewe na mumewe.