nawe ukaonesha ishara nyingi na mambo ya maajabu juu ya Farao, watumishi wake wote, na watu wote wa nchi yake; kwa maana ulijua ya kuwa waliwatenda kwa kutakabari; ukajipatia jina linalodumu hata leo.
Zaburi 78:43 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Alivyoziweka ishara zake katika Misri, Na miujiza yake katika uwanda wa Soani. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema alipotenda maajabu nchini Misri, na miujiza kondeni Soani! Biblia Habari Njema - BHND alipotenda maajabu nchini Misri, na miujiza kondeni Soani! Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza alipotenda maajabu nchini Misri, na miujiza kondeni Soani! Neno: Bibilia Takatifu siku aliyoonesha ishara zake za ajabu huko Misri, maajabu yake huko Soani. Neno: Maandiko Matakatifu siku aliyoonyesha ishara zake za ajabu huko Misri, maajabu yake huko Soani. BIBLIA KISWAHILI Alivyoziweka ishara zake katika Misri, Na miujiza yake katika uwanda wa Soani. |
nawe ukaonesha ishara nyingi na mambo ya maajabu juu ya Farao, watumishi wake wote, na watu wote wa nchi yake; kwa maana ulijua ya kuwa waliwatenda kwa kutakabari; ukajipatia jina linalodumu hata leo.
BWANA akamwambia Musa, Hapo utakaporudi Misri, angalia ukazifanye mbele ya Farao zile ajabu zote nilizozitia mkononi mwako; lakini nitaufanya mgumu moyo wake, naye hatawapa ruhusa hao watu waende zao.
Nami nitaufanya mgumu moyo wa Farao, nami nitazifanya kuwa nyingi ishara zangu na ajabu zangu katika nchi ya Misri.
Na lile taifa watakaowafanya watumwa nitawahukumu mimi, alisema Mungu; na baada ya hayo watatoka, nao wataniabudu mahali hapa.
Au Mungu amekwenda wakati gani akajitwalia taifa kutoka kati ya taifa lingine, kwa majaribu, ishara, maajabu, vita, mkono hodari, mkono ulionyoshwa, na vitisho vikuu, kama vile BWANA, Mungu wenu, alivyowatendea ninyi katika Misri, mbele ya macho yenu?
BWANA akaonesha ishara na maajabu makubwa na mazito, juu ya Misri, Farao, na nyumba yake yote, mbele ya macho yetu;