Zaburi 78:42 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Hawakuukumbuka mkono wake, Wala siku ile alipowakomboa na mtesi. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Hawakuikumbuka nguvu yake, wala siku ile alipowaokoa na maadui zao, Biblia Habari Njema - BHND Hawakuikumbuka nguvu yake, wala siku ile alipowaokoa na maadui zao, Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Hawakuikumbuka nguvu yake, wala siku ile alipowaokoa na maadui zao, Neno: Bibilia Takatifu Hawakukumbuka uwezo wake, siku aliyowakomboa kutoka kwa mtesi, Neno: Maandiko Matakatifu Hawakukumbuka uwezo wake, siku aliyowakomboa kutoka kwa mtesi, BIBLIA KISWAHILI Hawakuukumbuka mkono wake, Wala siku ile alipowakomboa na mtesi. |
Nayo itakuwa ishara kwako katika mkono wako, na kwa ukumbusho kati ya macho yako, ili kwamba sheria ya BWANA ipate kuwa kinywani mwako; kwani BWANA alikuondoa utoke Misri kwa mkono wenye uwezo.
Neno hili silo tulilokuambia huko Misri, tukisema, Tuache tuwatumikie Wamisri? Maana ni afadhali kuwatumikia Wamisri kuliko kufa jangwani.
Na itakuwa katika siku hiyo, Bwana atapeleka mkono wake mara ya pili, ili ajipatie watu wake watakaosalia, kutoka Ashuru, na kutoka Misri, na kutoka Pathrosi, na kutoka Kushi, na kutoka Elamu, na kutoka Shinari, na kutoka Hamathi, na kutoka visiwa vya bahari.
ukawatoa watu wako, Israeli, katika nchi ya Misri, kwa ishara, na kwa ajabu, na kwa mkono hodari, na kwa mkono ulionyoshwa, na kwa utisho mkuu;
Kwani wana wa Israeli hawakumkumbuka BWANA, Mungu wao, ambaye ndiye aliyewaokoa na mikono ya adui zao wote pande zote;