Zaburi 78:40 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Walimwasi jangwani mara ngapi? Na kumhuzunisha nyikani! Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mara ngapi walimwasi kule jangwani, na kumchukiza hukohuko nyikani! Biblia Habari Njema - BHND Mara ngapi walimwasi kule jangwani, na kumchukiza hukohuko nyikani! Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mara ngapi walimwasi kule jangwani, na kumchukiza hukohuko nyikani! Neno: Bibilia Takatifu Mara ngapi walimwasi jangwani na kumhuzunisha nyikani! Neno: Maandiko Matakatifu Mara ngapi walimwasi jangwani na kumhuzunisha nyikani! BIBLIA KISWAHILI Walimwasi jangwani mara ngapi? Na kumhuzunisha nyikani! |
Naam, wasiwe kama baba zao, Kizazi cha ukaidi na uasi. Kizazi kisichojitengeneza moyo, Wala roho yake haikuwa amini kwa Mungu.
Lakini wakaasi, wakamhuzunisha Roho yake Mtakatifu; kwa hiyo akawageukia, akawa adui, akapigana nao.
Naye akasema, Sikilizeni sasa, enyi nyumba ya Daudi; Je! Ni neno dogo kwenu kuwachosha wanadamu, hata mkataka kumchosha Mungu wangu pia?
BWANA akamwuliza Musa, Je! Watu hawa watanidharau hadi lini? Wasiniamini hadi lini? Nijapokuwa nimefanya ishara hizo zote kati yao.
Wala msimhuzunishe yule Roho Mtakatifu wa Mungu; ambaye kwa yeye mlitiwa mhuri hata siku ya ukombozi.
Kumbuka, usisahau ulivyomtia BWANA, Mungu wako, kasirani jangwani; tangu siku uliyotoka nchi ya Misri hadi mlipofika mahali hapa, mmekuwa na uasi juu ya BWANA