BWANA akasema, Roho yangu haitashindana na mwanadamu milele, kwa kuwa yeye naye ni mwili; basi siku zake zitakuwa miaka mia moja na ishirini.
Zaburi 78:39 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Akakumbuka ya kuwa wao ni kiwiliwili, Upepo upitao wala haurudi. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Alikumbuka kwamba wao ni watu tu; ni kama upepo upitao na kutoweka. Biblia Habari Njema - BHND Alikumbuka kwamba wao ni watu tu; ni kama upepo upitao na kutoweka. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Alikumbuka kwamba wao ni watu tu; ni kama upepo upitao na kutoweka. Neno: Bibilia Takatifu Alikumbuka kwamba wao walikuwa nyama tu, upepo upitao ambao haurudi. Neno: Maandiko Matakatifu Alikumbuka kwamba wao walikuwa nyama tu, upepo upitao ambao haurudi. BIBLIA KISWAHILI Akakumbuka ya kuwa wao ni kiwiliwili, Upepo upitao wala haurudi. |
BWANA akasema, Roho yangu haitashindana na mwanadamu milele, kwa kuwa yeye naye ni mwili; basi siku zake zitakuwa miaka mia moja na ishirini.
Kumbuka, nakusihi ulivyonifinyanga kama vile udongo; Nawe, je! Utanirudisha uvumbini tena?
lakini hamjui yatakayokuwako kesho. Uzima wenu ni nini? Maana ninyi ni mvuke uonekanao kwa muda mfupi tu, kisha hutoweka.