Zaburi 78:36 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Lakini walimdanganya kwa vinywa vyao, Wakamwambia uongo kwa ndimi zao. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Lakini walimdanganya kwa maneno yao; kila walichomwambia kilikuwa uongo. Biblia Habari Njema - BHND Lakini walimdanganya kwa maneno yao; kila walichomwambia kilikuwa uongo. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Lakini walimdanganya kwa maneno yao; kila walichomwambia kilikuwa uongo. Neno: Bibilia Takatifu Lakini walimdanganya kwa vinywa vyao, wakisema uongo kwa ndimi zao, Neno: Maandiko Matakatifu Lakini walimdanganya kwa vinywa vyao, wakisema uongo kwa ndimi zao, BIBLIA KISWAHILI Lakini walimdanganya kwa vinywa vyao, Wakamwambia uongo kwa ndimi zao. |
Bwana akanena, Kwa kuwa watu hawa hunikaribia na kuniheshimu kwa vinywa vyao, bali mioyo yao wamefarakana nami, na kicho chao walichonacho kwangu ni maagizo ya wanadamu waliyofundishwa;
Tena ni nani uliyemwogopa na kumhofu, hata ukasema uongo, wala hukunikumbuka mimi, wala kuweka hayo moyoni? Je! Mimi sikunyamaza tangu zamani, hata huniogopi?
Likiwa jema, au likiwa baya, sisi tutaitii sauti ya BWANA, Mungu wetu, ambaye tunakutuma kwake; ipate kuwa faida yetu, tunapoitii sauti ya BWANA, Mungu wetu.
Nao huja kwako kama watu wajavyo, nao hukaa mbele yako kama watu wangu, nao husikia maneno yako, wasiyatende; maana kwa vinywa vyao hujifanya kuwa wenye upendo mwingi, lakini mioyo yao inatafuta faida yao.
Efraimu amenizunguka kwa maneno ya uongo, na nyumba ya Israeli kwa udanganyifu; na Yuda hata sasa anasitasita kwa Mungu, na kwake aliye Mtakatifu, naye ni mwaminifu.
Efraimu hujilisha upepo, na kuandamana na upepo wa mashariki; haachi kuongeza uongo na uharibifu; nao wafanya agano na Ashuru, na mafuta huchukuliwa kwenda Misri.
BWANA naye ana shutuma juu ya Yuda, naye atamwadhibu Yakobo kwa kadiri ya njia zake; kwa kadiri ya matendo yake atamlipa.
Kwa maana matajiri wake wamejaa jeuri, na wenyeji wake wamesema uongo, na ulimi wao una udanganyifu kichwani mwao.