Ndiye apandishaye mvuke toka miisho ya nchi; Huifanyia mvua umeme; Hutoa upepo katika ghala zake.
Zaburi 78:26 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Aliuelekeza upepo wa mashariki kuvuma toka mbinguni; Na kwa uweza wake akauongoza upepo wa kusini. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Alivumisha upepo wa mashariki, kwa nguvu yake akachochea pepo za kusini; Biblia Habari Njema - BHND Alivumisha upepo wa mashariki, kwa nguvu yake akachochea pepo za kusini; Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Alivumisha upepo wa mashariki, kwa nguvu yake akachochea pepo za kusini; Neno: Bibilia Takatifu Aliachia upepo wa mashariki kutoka mbingu na kuuongoza upepo wa kusini kwa uwezo wake. Neno: Maandiko Matakatifu Aliachia upepo wa mashariki kutoka kwenye mbingu na kuuongoza upepo wa kusini kwa uwezo wake. BIBLIA KISWAHILI Aliuelekeza upepo wa mashariki kuvuma toka mbinguni; Na kwa uweza wake akauongoza upepo wa kusini. |
Ndiye apandishaye mvuke toka miisho ya nchi; Huifanyia mvua umeme; Hutoa upepo katika ghala zake.
Basi Musa akainyosha fimbo yake juu ya nchi ya Misri, na BWANA akaleta upepo kutoka mashariki juu ya nchi, mchana kutwa, na usiku kucha; kulipopambazuka ule upepo wa mashariki ukawaleta nzige.
Kisha upepo ukavuma kutoka kwa BWANA, nao ukaleta kware kutoka pande za baharini, nao ukawaacha wakaanguka karibu na kambi, kama kiasi cha mwendo wa siku moja upande huu, na kama kiasi cha mwendo wa siku moja upande ule, kuizunguka, nao wakafikia kiasi cha dhiraa mbili juu ya uso wa nchi.
Kisha hapo hiyo nyama ilipokuwa ikali kati ya meno yao, hawajaitafuna bado, hasira za BWANA ziliwaka juu ya watu, BWANA akawapiga watu kwa pigo kuu mno.