Ukawapa chakula toka mbinguni, kwa ajili ya njaa yao, na kwa ajili yao ukaleta maji kutoka mwambani, kwa sababu ya kiu yao, ukawaamuru waingie na kuimiliki, nchi ambayo umeinua mkono wako kuwapa.
Zaburi 78:24 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Akawanyeshea mana ili wale; Akawapa nafaka ya mbinguni. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema akawanyeshea mana wale, akawapa nafaka kutoka mbinguni. Biblia Habari Njema - BHND akawanyeshea mana wale, akawapa nafaka kutoka mbinguni. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza akawanyeshea mana wale, akawapa nafaka kutoka mbinguni. Neno: Bibilia Takatifu akawanyeshea mana ili watu wale; aliwapa nafaka ya mbinguni. Neno: Maandiko Matakatifu akawanyeshea mana ili watu wale; aliwapa nafaka ya mbinguni. BIBLIA KISWAHILI Akawanyeshea mana ili wale; Akawapa nafaka ya mbinguni. |
Ukawapa chakula toka mbinguni, kwa ajili ya njaa yao, na kwa ajili yao ukaleta maji kutoka mwambani, kwa sababu ya kiu yao, ukawaamuru waingie na kuimiliki, nchi ambayo umeinua mkono wako kuwapa.
Ukawapa na roho yako mwema ili kuwaelimisha, wala hukuwanyima mana vinywani mwao, tena ukawapa maji kwa ajili ya kiu yao.
Na ulipokauka ule umande uliokuwa juu ya nchi, kumbe! Juu ya uso wa bara kitu kidogo kilichoviringana, kidogo kama barafu juu ya nchi.
Ndipo BWANA akamwambia Musa, Tazama, mimi nitawanyeshea ninyi mvua ya mkate kutoka mbinguni; na hao watu watatoka nje na kuokota kila siku sehemu ya siku; ili nipate kuwajaribu, kwamba watakwenda katika sheria yangu, ama sivyo.
Nami miaka arubaini nimewaongoza jangwani; nguo zenu hazikuchakaa juu yenu, wala kiatu chako hakikuchakaa katika mguu wako.
Akakunyenyekeza, akakuacha uone njaa, akakulisha kwa mana, usiyoijua wewe wala baba zako hawakuijua; apate kukujulisha ya kuwa mwanadamu haishi kwa mkate tu, bali huishi kwa kila litokalo katika kinywa cha BWANA.