Katika mwaka wa mia sita wa maisha ya Nuhu, mwezi wa pili, siku ya kumi na saba ya mwezi, siku ile chemchemi zote za vilindi vikuu zilibubujika kwa nguvu, madirisha ya mbinguni yakafunguka.
Zaburi 78:23 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Lakini aliyaamuru mawingu juu; Akaifungua milango ya mbinguni; Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Hata hivyo aliyaamuru mawingu ya juu, akaifungua milango ya mbingu; Biblia Habari Njema - BHND Hata hivyo aliyaamuru mawingu ya juu, akaifungua milango ya mbingu; Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Hata hivyo aliyaamuru mawingu ya juu, akaifungua milango ya mbingu; Neno: Bibilia Takatifu Hata hivyo alitoa amri kwa anga zilizo juu na kufungua milango ya mbingu, Neno: Maandiko Matakatifu Hata hivyo alitoa amri kwa anga zilizo juu na kufungua milango ya mbingu, BIBLIA KISWAHILI Lakini aliyaamuru mawingu juu; Akaifungua milango ya mbinguni; |
Katika mwaka wa mia sita wa maisha ya Nuhu, mwezi wa pili, siku ya kumi na saba ya mwezi, siku ile chemchemi zote za vilindi vikuu zilibubujika kwa nguvu, madirisha ya mbinguni yakafunguka.
na yule kiongozi akamjibu mtu wa Mungu, akasema, Sasa tazama, kama BWANA angefanya madirisha mbinguni, je! Jambo hili lingewezekana? Akasema, Angalia, wewe utaliona kwa macho yako, lakini hutakula.
Basi yule afisa, ambaye mfalme alikuwa akitegemea mkono wake, akamjibu yule mtu wa Mungu, akasema, Tazama, kama BWANA angefanya madirisha mbinguni, je! Jambo hili lingewezekana? Akamwambia, Angalia, wewe utaliona kwa macho yako, lakini hutakula.
nami nitaliharibu; wala halitapogolewa wala kulimwa, bali litamea mbigili na miiba; nami nitayaamuru mawingu yasinyeshe mvua juu yake.
Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema BWANA wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la.