Walakini hawakutaka kusikia, bali walifanya shingo zao kuwa ngumu, kama shingo za baba zao, wasiomwamini BWANA, Mungu wao.
Zaburi 78:22 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Kwa kuwa hawakumwamini Mungu, Wala hawakuutumainia wokovu wake. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema kwa sababu hawakuwa na imani naye, wala hawakuamini nguvu yake ya kuokoa. Biblia Habari Njema - BHND kwa sababu hawakuwa na imani naye, wala hawakuamini nguvu yake ya kuokoa. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza kwa sababu hawakuwa na imani naye, wala hawakuamini nguvu yake ya kuokoa. Neno: Bibilia Takatifu kwa kuwa hawakumwamini Mungu, wala kuutumainia ukombozi wake. Neno: Maandiko Matakatifu kwa kuwa hawakumwamini Mungu, wala kuutumainia ukombozi wake. BIBLIA KISWAHILI Kwa kuwa hawakumwamini Mungu, Wala hawakuutumainia wokovu wake. |
Walakini hawakutaka kusikia, bali walifanya shingo zao kuwa ngumu, kama shingo za baba zao, wasiomwamini BWANA, Mungu wao.
tena kichwa cha Efraimu ni Samaria, na kichwa cha Samaria ni mwana wa Remalia. Ikiwa hamtasimama imara katika imani, hamtathibitika kamwe.
Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao.
Hadharini, ndugu zangu, usiwepo katika mmoja wenu moyo mbovu wa kutoamini, ujitengao na Mungu aliye hai.
Yeye amwaminiye Mwana wa Mungu anao huo ushuhuda ndani yake. Asiyemwamini Mungu amemfanya kuwa mwongo, kwa kuwa hakuuamini huo ushuhuda ambao Mungu amemshuhudia Mwanawe.
Tena napenda kuwakumbusha, ijapokuwa mmekwisha kujua haya yote, ya kwamba Bwana, akiisha kuwaokoa watu katika nchi ya Misri, aliwaangamiza baadaye wale wasioamini.