Zaburi 78:15 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Akapasua miamba jangwani; Akawanywesha maji mengi kama maji ya vilindi. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Aliipasua miamba kule jangwani, akawanywesha maji kutoka vilindini. Biblia Habari Njema - BHND Aliipasua miamba kule jangwani, akawanywesha maji kutoka vilindini. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Aliipasua miamba kule jangwani, akawanywesha maji kutoka vilindini. Neno: Bibilia Takatifu Alipasua miamba jangwani na akawapa maji tele kama bahari, Neno: Maandiko Matakatifu Alipasua miamba jangwani na akawapa maji tele kama bahari, BIBLIA KISWAHILI Akapasua miamba jangwani; Akawanywesha maji mengi kama maji ya vilindi. |
Tazama, nitasimama mbele yako huko, juu ya lile jabali katika Horebu; nawe utalipiga jabali, na maji yatatoka, watu wapate kunywa. Musa akafanya hivyo mbele ya wazee wa Israeli.
Nitafunua vijito vya maji juu ya vilima, na chemchemi katikati ya mabonde; nitageuza jangwa kuwa ziwa la maji, na mahali pakavu kuwa vijito vya maji.
Wanyama pori wataniheshimu, mbweha pia na mbuni; kwa sababu nimewapa maji jangwani, na mito nyikani, ili kuwanywesha watu wangu, wateule wangu;
Wala hawakuona kiu alipowaongoza jangwani; Alitoa maji katika mwamba kwa ajili yao; Pia akaupasua mwamba, maji yakatoka kwa nguvu.
Musa akainua mkono wake akaupiga ule mwamba kwa fimbo yake mara mbili; maji yakatoka mengi, mkutano wakanywa na wanyama wao pia.
wote wakanywa kinywaji kile kile cha roho; kwa maana waliunywea mwamba wa roho uliowafuata; na mwamba ule ulikuwa ni Kristo.
Kisha akanionesha mto wa maji ya uzima, wenye kung'aa kama bilauri, ukitoka katika kiti cha enzi cha Mungu, na cha Mwana-kondoo,
Roho na Bibi arusi wasema, Njoo! Naye asikiaye na aseme, Njoo! Naye mwenye kiu na aje; na yeye atakaye, na ayatwae maji ya uzima bure.