Zaidi ya hayo ukawaongoza kwa nguzo ya wingu mchana; na kwa nguzo ya moto usiku; ili kuwapa mwanga katika njia iliyowapasa kuiendea.
Zaburi 78:14 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Akawaongoza kwa wingu mchana, Na usiku kucha kwa nuru ya moto. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Mchana aliwaongoza kwa wingu; usiku kucha kwa mwanga wa moto. Biblia Habari Njema - BHND Mchana aliwaongoza kwa wingu; usiku kucha kwa mwanga wa moto. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Mchana aliwaongoza kwa wingu; usiku kucha kwa mwanga wa moto. Neno: Bibilia Takatifu Aliwaongoza kwa wingu mchana, na kwa nuru ya moto usiku kucha. Neno: Maandiko Matakatifu Aliwaongoza kwa wingu mchana na kwa nuru kutoka kwenye moto usiku kucha. BIBLIA KISWAHILI Akawaongoza kwa wingu mchana, Na usiku kucha kwa nuru ya moto. |
Zaidi ya hayo ukawaongoza kwa nguzo ya wingu mchana; na kwa nguzo ya moto usiku; ili kuwapa mwanga katika njia iliyowapasa kuiendea.
hata hivyo wewe kwa wingi wa rehema zako hukuwaacha jangwani; nguzo ya wingu haikuondoka kwao wakati wa mchana, ili kuwaongoza njiani; wala nguzo ya moto haikuondoka wakati wa usiku, ili kuwapa mwanga na kuwaonesha njia watakayoiendea.
Ikawa katika zamu ya alfajiri, BWANA akalichungulia jeshi la Wamisri katika ile nguzo ya moto na ya wingu, akalifadhaisha jeshi la Wamisri.