Usiku ule mfalme hakupata usingizi; akaamuru aletewe kitabu cha kumbukumbu nacho kikasomwa mbele ya mfalme.
Zaburi 77:4 - Swahili Revised Union Version - SRUVDC Ulizishika kope za macho yangu zisifumbike; Nilitaabika nisiweze kunena. Matoleo zaidiBiblia Habari Njema Wanizuia hata kupata lepe la usingizi, nina mahangaiko hata kusema siwezi. Biblia Habari Njema - BHND Wanizuia hata kupata lepe la usingizi, nina mahangaiko hata kusema siwezi. Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza Wanizuia hata kupata lepe la usingizi, nina mahangaiko hata kusema siwezi. Neno: Bibilia Takatifu Ulizuia macho yangu kufumba; nilikuwa nasumbuka, nikashindwa kusema. Neno: Maandiko Matakatifu Ulizuia macho yangu kufumba; nilikuwa nasumbuka, nikashindwa kusema. BIBLIA KISWAHILI Ulizishika kope za macho yangu zisifumbike; Nilitaabika nisiweze kunena. |
Usiku ule mfalme hakupata usingizi; akaamuru aletewe kitabu cha kumbukumbu nacho kikasomwa mbele ya mfalme.
Kisha wakaketi ardhini pamoja naye muda wa siku saba, mchana na usiku, wala hapana mmoja aliyenena naye neno lolote; kwa maana waliona ya kuwa mashaka yake aliyo nayo ni makuu mno.
Kwa kuwa sasa ungekuwa mzito kuliko mchanga wa bahari; Kwa hiyo maneno yangu yamekuwa ya haraka.
Nimechoka kwa kuugua kwangu; Kila usiku nakibubujikia kitanda changu; Nililowesha godoro langu kwa machozi yangu.